Bata-maji
Bata-maji domo-fundo
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Anseriformes (Ndege kama bata)
Familia: Anatidae (Ndege walio na mnasaba na mabata)
Nusufamilia: Anserinae (Ndege wanaofanana na mabata bukini)
Vigors, 1825
Ngazi za chini

Jenasi 2, spishi 7:

Mabata-maji ni ndege wakubwa wa maji wa jenasi Cygnus katika familia ya Anatidae. Wanaainishwa katika nusufamilia Anserinae pamoja na mabata bukini. Mabata-maji ni ndege wakubwa kabisa wa familia yao wenye shingo ndefu na domo pana. Spishi za nusudunia ya kaskazini zina rangi nyeupe tu, lakini spishi za nusudunia ya kusini ni nyeupe na nyeusi. Hula mimea ya maji hasa lakini manyasi mafupi na wadudu pia. Tago lao limejengwa kwa matete na mimea ya maji juu ya nchi kavu lakini karibu sana ya maji.

Ndege hawa huzaana kwa kanda za kaskazini na kusini za dunia. Wakati wa majira ya baridi au ukavu huhama kanda za moto zaidi au ambapo mvua unanyesha. Spishi kadha, hususa Bata-maji Domo-fundo na Bata-maji Mweusi, zimewasilishwa nje ya eneo lao la usambazaji, k.m. Afrika ya Kusini.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri