Nusutufe ya kusini

(Elekezwa kutoka Nusudunia ya kusini)

Nusutufe ya kusini (pia nusudunia ya kusini; Kiing.: Southern Hemisphere) ni nusu ya Dunia ilioko upande wa kusini wa ikweta.

Nusutufe ya Kusini: Antaktika (katikati), Amerika Kusini (juu kushoto), Afrika (juu kulia), Australia na eneo la Pasifiki
Bango lililoandikwa: "Ushuaia, mwisho wa ulimwengu". Ushuaia huko Argentina ndio mji wa kusini kabisa ulimwenguni.
Tofauti ya viwango vya bahari na nchi kavu kati ya nusutufe mbili za dunia.

Tofauti na nusutufe ya kaskazini hii ya kusini ina maeneo makubwa zaidi ya bahari ambayo ni asilimia 80.9, ilhali kaskazini ni asilimia 60.7 pekee. Theluthi moja tu, yaani 32.7%, za nchi kavu ya Dunia iko kwenye nusutufe ya kusini.[1]

Kati ya mabara ni Antaktiki na Australia nzima, asilimia 90 za Amerika Kusini na theluthi ya kusini ya Afrika yaliyopo kwenye nusutufe hiyo. Kuna pia visiwa vikubwa vya Asia kusini kwa ikweta na visiwa vingi vya Pasifiki. [2]

Majira ya joto ni kuanzia Disemba hadi Machi, na majira ya baridi kuanzia Juni hadi Septemba.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Life on Earth: A - G.. 1. ABC-CLIO. 2002. uk. 528. ISBN 9781576072868. Iliwekwa mnamo 8 Septemba 2016.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Life on Earth: A - G.. 1. ABC-CLIO. 2002. uk. 528. ISBN 9781576072868. Iliwekwa mnamo 8 Septemba 2016.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)