Becky Anderson

Mwandishi wa habari wa Uingereza

Becky Anderson (alizaliwa 15 Novemba 1967) ni mwandishi wa habari Mwingereza, na mtangazaji wa CNN International kwenye kipindi cha "Connect the World with Becky Anderson".

Anderson akiwa kwenye mkutano wa World Economic Forum mjini Davos

Anderson ana shahada ya Uchumi na Kifaransa kutoka Chuo Kikuu cha Sussex, na shahada ya pili ya Uanahabari kutoka Chuo Kikuu cha Arizona State. Ameanza kazi kama mwandishi wa habari kwa kufanya kazi mjini Arizona mnamo mwaka wa 1990, na pindi alipoanza kazi CNN mwaka 1999, alikuwa akitangaza World Business This Morning. Yeye ni mtangazaji wa CNN International kutoka afisi ya London.

Mtazamo wake ulikuwa kwenye taarifa za kifedha lakini amepanua mada yake na kuzingatia maandamano ya Kifaransa iliyotokea mapema mnamo 2006. Taarifa yake ni yenye muelekeo wa moja kwa moja na wa kusisimua.

Anderson ni shabiki wa Tottenham Hotspur.

Viungo vya nje hariri