Bees for Development
Bees for Development ni shirikisho la misaada la kimataifa, maalumu kwa kazi ya kupunguza umaskini kwa njia ya ufugaji nyuki. Ufugaji nyuki unachangia kusaidia maslahi endelevu ya kuishi katika jumuiya za maskini na nyuki kutoa huduma muhimu ya mazingira bora ya kuishi. Bees for Development inaendesha miradi Uganda, Zanzibar, Ethiopia na Kirgizia. Ofisi zake ziko Monmouth, Wales Kusini.
Historia na falsafa
haririIlianzishwa mwaka wa 1993, inafanya kazi kwa kushirikiana na waweka nyuki na mashirika ya kimataifa,kama vile Apimondia, Wakfa wa Keystone na shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa.Ufadhili huu unakusudia kusaidia ufugaji nyuki ili kusaidia jamii maskini na vivjiji vilivyo mashinani na kulinda viumbe hai.Inalenga matumizi ya teknolojia sahihi na maadili, na kuheshimu ujuzi wa kienyeji. Ina imani kuwa kujitegemea na kuwawezesha maskini kunaweza kuimarishwa kwa njia ya upatikanaji wa maarifa na habari, na kwa njia ya biashara ya mazao ya nyuki.Pia inadai kuingilia uzalishaji wa nyuki kuwa kiwango cha chini kabisa, na thamani ya kutumia mizinga ambayo haina fremu za ndani.
Shughuli
haririJarida la Bees for Development linachapishwa kila baada ya miezi mitatu.Linaangazia teknolojia mwafaka za ufugaji nyuki, kubadilishana masomo yaliyosomwa katika nchi mbalimbali, na inajumuisha taarifa ya kisasa kuhusu ufugaji nyuki duniani kote. Mradi wa Biashara ya Asali wa Uganda pamoja na vyama vya wafuga nyuki wa kiasili pamoja na ApiTrade Afrika, kusaidia kukuza mapato kwa njia ya kuimarisha biashara ya asali. Huko Zanzibar Bees for Development inatekeleza mradi wa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la Denmark, DANTAN, ikiangazia kutia nguvu sekta ya asali huko Unguja, kisiwa kikuu cha Zanzibar na katika kisiwa cha Pemba. Huko Kirgizia, fedha kutoka Mpango wa Darwin, ambao hupea moyo viumbe hai katika nchi maskini zimepatikana, na Bees for Development inafanya kazi na Wakfu wa Maendeleo Vijijini kusaidia wafuga nyuki kufikia haki ya kupata ardhi ya malisho ya ufugaji nyuki. Bees for Development pia inasambaza rasilimali za mafunzo duniani kote, inasimamia maktaba maktaba ya mtandao yenye habari kuhusu ufugaji wa nyuki na safari za kwenda kujionea ufugaji wa nyuki huko Trinidad, Tobago,na Uturuki.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
Viungi Vya nje
hariri- Bees for Development Website
- ApiTrade Africa and their youtube channel
- UEPB Ilihifadhiwa 2 Aprili 2013 kwenye Wayback Machine.
- TUNADO