Trinidad na Tobago
Jamhuri ya Trinidad na Tobago ni nchi ya visiwani katika Karibi ya kusini, karibu na pwani ya Venezuela, kusini kwa kisiwa cha Grenada cha Antili Ndogo. Nchi jirani nyingine kuvukia bahari ni Barbados na Guyana.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Together we aspire, together we achieve | |||||
Wimbo wa taifa: Forged From The Love of Liberty | |||||
Mji mkuu | Port of Spain | ||||
Mji mkubwa | Chaguanas [1] | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali | Jamhuri Paula-Mae Weekes Keith Rowley | ||||
Uhuru Kutoka Uingereza |
31 Agosti 1962 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
5,131 km² (ya 165) Kidogo sana | ||||
Idadi ya watu - Julai 2019 kadirio - Msongamano wa watu |
1,363,985 (ya 151) 264/km² (ya 54) | ||||
Fedha | Trinidad and Tobago dollar (TTD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-4) (UTC n/a) | ||||
Intaneti TLD | .tt | ||||
Kodi ya simu | +1-868
- |
Nchi ina eneo la km² 5,128 ambalo karibu lote ni kisiwa kikuu cha Trinidad. Kile cha Tobago kina asilimia 6 tu za eneo pamoja na 4% ya wakazi. Kuna visiwa vidogo vingine 21.
Ni jamhuri mwanachama wa Jumuiya ya Madola.
Ni nchi iliyoendelea, ikishika nafasi ya tatu kati ya zile za Amerika baada ya Marekani na Kanada.
Historia
haririVisiwa vilikaliwa na Waindio kwa karne nyingi kabla ya ujio wa Kristofa Columbus na Wahispania (1498).
Trinidad ilibaki chini ya wakoloni hao hadi mwaka 1797 vilipotekwa na Waingereza ambao walikabidhiwa pia Tobago mwaka 1802. Viliunganishwa mwaka 1889 na kubaki koloni hadi mwaka 1962 vilipopata uhuru.
Watu
haririWakazi wengi wana asili ya India (37.6%), lakini pia ya Afrika (36.3%) na sehemu nyingine. Hivyo kuna machotara wa aina mbalimbali (24.2%).
Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini wananchi wengi wanaongea kwa kawaida aina mbili za Krioli. Asilimia 5 wanaongea Kihispania.
Upande wa dini wengi (63%) ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Kanisa Katoliki (21.5%), Wapentekoste (12%) na Anglikana (5.7%). Wahindu ni 18% na Waislamu ni 5%.
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Trinidad and Tobago Government Portal
- Official Trinidad and Tobago Tourism Company Website
- Trinidad and Tobago entry at The World Factbook
- Trinidad and Tobago Archived 6 Septemba 2012 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- and Tobago/ Trinidad na Tobago katika Open Directory Project
- Trinidad and Tobago profile from the BBC News
- World Bank Summary Trade Statistics Trinidad and Tobago
- Wikimedia Atlas of Trinidad and Tobago
- Key Development Forecasts for Trinidad and Tobago from International Futures
- Guanaguanare – the Laughing Gull. Carib Indians in Trinidad – includes 2 videos
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Trinidad na Tobago kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |