Beginnings: The Lost Tapes 1988–1991
Beginnings: The Lost Tapes 1988–1991 ni jina la kutaja albamu ya msanii wa rekodi za muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani, 2Pac. Albamu ilitolewa baada ya kifo chake - mnamo tar. 12 Juni, 2007[1][2][3] kupitia studio za Koch Records. Awali albamu ilitolewa mnamo tar. 18 Aprili, 2000 katika muundo wa bootleg, chini ya jina la The Lost Tapes: Circa 1989, lakini mauzo yake yalisimamishwa mara moja kutokana na tatizo la ukiukaji wa hatimiliki.
Beginnings: The Lost Tapes 1988-1991 | |||||
---|---|---|---|---|---|
Compilation album ya 2Pac | |||||
Imetolewa | Juni 12, 2007 (Marekani)[1][2][3] | ||||
Aina | Hip-hop | ||||
Lebo | Koch | ||||
Mtayarishaji | Chopmaster J | ||||
Wendo wa albamu za 2Pac | |||||
|
Albamu ilitayarishwa na mmoja wa wanakundi la Digital Underground, Chopmaster J, [4] Beginnings... ni mkusanyiko wa nyimbo zake za mwanzoni kabisa, ilitengenezwa kabla Shakur hajaanza kuifanyia kazi albamu yake ya kwanza, 2Pacalypse Now. [4]
Mapokezi ya haja
haririMakadirio ya kitaalamu | |
---|---|
Tahakiki za ushindi | |
Chanzo | Makadirio |
Allmusic | [Beginnings: The Lost Tapes 1988–1991 katika Allmusic link] |
CD Universe walieleza ya kwamba "uimbaji wa Shakur na maudhui ya mashairi yake ni kumbukumbu ya waimbaji waliotamba mwisho/mwanzoni mwa miaka ya 1980s/1990 kama kina Big Daddy Kane na Rakim" kuliko hata nyimbo zake mwenyewe 2Pac za baadaye.[2] Jason Birchmeier wa Allmusic alikubali ya kwamba rapa huyu anaonekana "kuvutia zaidi hapa, shaka hakuna, lakini hata hivyo mzito kidogo na anagezea".[4] Birchmeier nae pia alieleza yake ya kwamba "kuna jambo hapa kidogo kuliko lile fuvu la mashine ya utayarishaji wa biti".[4]
Orodha ya nyimbo
hariri- "Panther Power" 4:36
- "The Case of the Misplaced Mic" 2:34
- "Let Knowledge Drop" 3:37
- "Never Be Beat" 5:33
- "A Day in the Life" 4:55
- "My Burnin' Heart" 6:25
- "Minnie the Moocher" 4:19
- "The Case of the Misplaced Mic, Pt. 2" 2:40
- "Static Mix, Pt. 1" 4:19
- "Static Mix, Pt. 2" 3:59
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 "Tupac Shakur Beginnings : The Lost Tapes 1988-1991 - Hip Hop Galaxy". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-17. Iliwekwa mnamo 2013-10-01.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 Tupac Shakur Beginnings: Lost Tapes 1988-1991 CD
- ↑ 3.0 3.1 Amazon.com: Beginnings The Lost Tapes 1988-1991: Music: Tupac Shakur
- ↑ 4.0 4.1 4.2 4.3 Birchmeier, Jason. "The Lost Tapes - 2Pac". Allmusic. Iliwekwa mnamo Septemba 25, 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya Nje
hariri- 2Pac Legacy (Official website)
- Tupac Amaru Shakur Foundation for the Arts