Pac's Life
Pac's Life ni jina la kutaja albamu ya tano kutolewa baada ya kifo cha hayati Tupac Shakur, ukumbusho wa maadhimisho ya miaka kumi ya kifo chake. Albamu ilitolewa mnamo tar. 21 Novemba 2006, huko nchini Marekani, kupitia Amaru Entertainment na Interscope Records. Japokuwa imeuza vizuri dunia nzima, lakini albamu imefeli kupata kushinda Dhahabu huko nchini Marekani.
Pac's Life | |||||
---|---|---|---|---|---|
Studio album ya 2Pac | |||||
Imetolewa | 21 Novemba 2006 20 Novemba 2006 18 Novemba 2006 13 Desemba 2006 [1] |
||||
Imerekodiwa | 1995-1996 (2Pac and Yaki Kadafi vocals) 2006 (added guest vocals) |
||||
Aina | West Coast hip hop, Rap, Gangsta rap | ||||
Lebo | Amaru/Interscope | ||||
Mtayarishaji | Afeni Shakur (exec.), Canei Finch, E.D.I., Karma Productions, L. T. Hutton, QD3, Salih, Sha Money XL, Swizz Beatz, Tom Whalley (exec.) | ||||
Tahakiki za kitaalamu | |||||
|
|||||
Wendo wa albamu za 2Pac | |||||
|
Historia
haririAlbamu imeuzisha sura kutoka kwa msanii kama vile Ashanti na T.I., ambaye ameonekana kwenye kibao cha "Pac's Life", na Krayzie Bone, ambaye ameonekana kwenye single ya kwanza ya albamu, "Untouchable".
Safu kubwa ya wasanii wamechangia katika albamu, ikiwa ni pamoja na Ashanti, T.I., Snoop Dogg, Ludacris, Bone Thugs-N-Harmony, Papoose, Keyshia Cole, Chamillionaire, Lil' Scrappy, Big Syke, Young Buck, Outlawz, ikiwa ni pamoja na mwonekano wa awali wa Yaki Kadafi, na Jamal Woolard, ambaye amekuja kuwa maarufu baada ya kuigiza kama The Notorious B.I.G. kwenye filamu kuhusu uhai wa maisha ya Big Small mnamo 2009 kwenye Notorious.
T.I. na Ashanti walishirikishwa kwenye single ya "Pac's Life," ambayo video yake ilifanyiwa katika Tupac Amaru Shakur Center for the Arts. Utambulisho wa Kimataifa wa "Pac's Life" ulirushwa saa 7:30 PM kupitia BET Access Granted kunako Jumatano, 22 Novemba. Video inaonesha matukio ya BET kwa nyuma wakati wa kutengeneza filamu ya "Pac's Life". Albamu ilishika nafasi ya #9 kwenye chati za Billboard 200 ikiwa na nakala 159,000 iliouza nchini Marekani katika wiki yake ya kwanza. Albamu mpaka sasa imeuza nakala zaidi ya 400,000 kuanzia mwezi wa Juni 2007, na kwa makadirio ya sasa yamefikia kiasi cha 500,000. Albamu imeuza kiasi chake dunia nzima, ingawa idadi kamili ya mauzo yake bado hayajulikani. Pia kumekuwa na funnu za kwamba, wamemlipa Ashanti zaidi ya milioni 3 ili aweze kuonekana kwenye single na video yake kwa ujumla, ilitajwa na mama'ke.
Hii ilikuwa albamu ya sita kutengenezwa baada ya kifo cha Shakur, lakini sio ya mwisho, albamu nyingine imepangwa itolewe mnamo mwezi wa Juni 2010. Mnamo mwezi wa Juni 2008 Death Row Records wameuza pamoja haki zaidi ya nyimbo 13 za Tupac ambazo hazikutolewa.
Orodha ya nyimbo
hariri# | Jina | Mtayarishaji | Muda |
---|---|---|---|
1 | "Untouchable" (Swizz Beatz Remix) (akimshirikisha: Krayzie Bone) | Johnny J - Imeremixiwa na Swizz Beatz | 4:16 |
2 | "Pac's Life" (akimshirikisha: Ashanti, T.I.) | Johnny J - Imeremixiwa na L. T. Hutton | 3:38 |
3 | "Dumpin'" (akimshirikisha: Hussein Fatal, Papoose, Carl Thomas) - (Awali ilishirikisha: Tha Dogg Pound, Kausin, Scarla) | Daz Dillinger - Imeremixiwa na Sha Money XL, Canei Finch | 4:27 |
4 | "Playa Cardz Right (Toleo la Kike)" (akimshirikisha: Keyshia Cole) - (Awali ilishirikisha: K-Ci na JoJo, Big Syke, Mopreme) | Johnny J - Imeremixiwa na Karma Productions | 4:33 |
5 | "What'z Next?" (akimshirikisha: A3, Jay Rock) - (Awali ilishirikisha: Big Syke, Mopreme) | Johnny J - Imeremixiwa na Salih Williams | 3:37 |
6 | "Sleep" (akimshirikisha: Young Buck, Chamillionaire) - (Awali ilishirikisha: Outlawz) | Daz Dillinger - Imeremixiwa na Sha Money XL | 4:10 |
7 | "International" (akimshirikisha: Nipsey Hussle, Young Dre The Truth) - (Awali ilishirikisha: Boot Camp Click) | L.T. Hutton | 4:01 |
8 | "Don't Sleep" (akimshirikisha: Lil Scrappy, Nutt-So, Kadafi, Stormy) - (Awali ilishirikisha: Outlawz, Nutt-So, Lil' Big) | Go-Twice - Imeremixiwa na E.D.I. | 3:36 |
9 | "Soon As I Get Home" (akimshirikisha: Kadafi) - (Awali ilishirikisha: Kadafi) | QD3 | 3:40 |
10 | "Playa Cardz Right (Male Version)" (akimshirikisha: Ludacris, Keon Bryce) (Awali ilishirikisha: K-Ci na JoJo, Big Syke, Mopreme) | Johnny J - Imeremixiwa na Sha Money XL | 4:54 |
11 | "Don't Stop" (akimshirikisha: Big Syke, Kadafi, Hussein Fatal, Young Noble, Stormy, E.D.I.) - (Awali ilishirikisha: Outlawz) | Johnny J - Imeremixiwa na L.T. Hutton | 5:25 |
12 | "Pac's Life" (Remix) (akimshirikisha: Snoop Dogg, Chris Starr, T.I.) | Johnny J - Imeremixiwa na L. T. Hutton | 3:39 |
13 | "Untouchable" (akimshirikisha: Kadafi, Hussein Fatal, Gravy) | Johnny J - Imeremixiwa na Sha Money XL | 4:25 |
Historia ya chati
haririChati (2006)[2] | Nafasi |
---|---|
U.S. Billboard 200 | 9 |
U.S. Billboard Top R&B/Hip-Hop Albums | 3 |
U.S. Billboard Top Rap Albums | 3 |
Marejeo
hariri- ↑ http://www.hmv.co.jp/product/detail/1213183 Album Listing (JP)
- ↑ ((( Pac's Life > Charts & Awards > Billboard Albums ))). All Media Guide, LLC. Retrieved on 2010-01-30.