Bendera ya Tajikistan

Bendera ya Tajikistan imepatikana tangu mwaka 1992 yaani mwaka mmoja baada ya uhuru wa Tajikistan. Ina milia mitatu ya nyekundu, nyeupe na kijani. Mlia mweupe ni pana kuliko milia mingine. Katikati kuna alama ya rangi dhahabu ya taji lenye nyota saba.

Bendera ya Tajikistan
Bendera ya Jamhuri ya Kisoviet ya Tajikistan ndani ya Umoja wa Kisoviet 1953 - 1991

Rangi za bendera ni sawa na rangi za bendera ya Uajemi. Utamaduni na lugha za nchi hizi mbili ni karibu sana.