Benki Kuu ya Mauritius

Benki ya Mauritius ni benki kuu ya Jamhuri ya Mauritius. Ilianzishwa mnamo Septemba 1967 kama benki kuu ya Mauritius. Iliundwa kwa mfano wa Benki Kuu ya Uingereza, na hivyo iliundwa kwa msaada wa maafisa wa Benki Kuu ya Uingereza.

Benki Kuu ya Mauritius
New Bank of Mauritius Tower
New Bank of Mauritius Tower
Headquarters {{{headquarters}}}
Central bank of Mauritius
ISO 4217 Code MUR
Website bom.intnet.mu

Miongoni mwa majukumu yake ni kutoa sarafu ya Mauritius, Rupia ya Mauritius.

Historia

hariri

Katika karne ya 19 benki tatu tofauti, kwa sasa zimeisha, zilifanya kazi chini ya jina la Benki Kuu ya Mauritius.

Benki Kuu ya kwanza ya Mauritius ilianza shughuli katika mwaka wa 1813 au hivyo, lakini iliishi tu mpaka 1825.

Benki ya pili ya Mauritius ilikuwa benki ya ng'ambo ya Uingereza ikiwa na bodi za wakurugenzi mbili, moja mjini London na nyingine Port Louis. Ilianza shughuli zake mwakani 1832 na ikapendeza maslahi ya wakulima.

Mwakani 1838 wafanyabiashara walianzisha Commercial Bank Mauritius ili kujipatia mbadala wa chanzo cha mikopo kwani tangu kuanzishwa kwake, Benki Kuu ya Mauritius ilikuwa benki ya pekee katika kisiwa hicho. Tatizo la kifedha la 1847 mjini London lilisababisha kuanguka kwa soko la sukari, na hasara kubwa kwa mabenki yote mawili ya Mauritius. Benki Kuu ya Mauritius iliacha biashara mwakani 1848, ingawa Mauritius Commercial Bank imeishi mpaka waleo.

Wawakezaji wa ndani walianzisha Benki ya Mauritius ya tatu mwakani 1894 ili kuchukua biashara ya ndani ya benki iliyoanguka ya New Oriental Corporation. Mwakani 1911, benki hii ilifungua tawi nchini Shelisheli. Hata hivyo, mwakani 1916 Benki ya Mercantile ya India (est 1893) iliinunua benki hii. HSBC kwa upande mwingine iliinunua Benki Mercantile mwakani 1959. Kwa sababu hii ya historia, HSBC hujiita benki kongwe zaidi ya kigeni nchini Mauritius. Benki ya kigeni iliyowasili baadaye, na imeishi hadi sasa, ilikuwa ni Benki ya Taifa ya Afrika ya Kusini, ambayo iliizaa Benki ya Barclays Mauritius.

Kuongezea mabenki haya matatu, benki kwa jina la Colonial Bank of Mauritius, Bourbon, and Dependencies, iliendesha shughuli zake kati ya 1812 na 1813.

Bodi ya Makamishna wa sarafu

hariri

Kabla ya uanzishwaji wa Benki, suala la sarafu lilikuwa linasimamiwa na Bodi ya Makamishna wa Fedha. Majukumu ya Bodi yalikuwa tu ya kutoa mamlaka. Uundaji wa Benki Kuu ya Mauritius ulikuwa mwanzo wa awamu mpya katika historia ya fedha ya Mauritius, kwa mfumo wa fedha kusonga mbele kutoka kwenye kiwango cha 'Sterling Exchange Standard', ambacho sarafu ilibadilishwa kwa Sterling katika kiwango sawa, na kuwa 'managed currency' ambacho jukumu huru la mamlaka ya fedha huwa muhimu.

Malengo ya Benki

hariri

Kipengele cha sheria cha Benki Kuu ya Mauritius cha 1966 (kama ilivyorekebishwa) kinaelezea makusudi ya benki hii ambayo ni 'kulinda thamani ya ndani na nje ya sarafu ya Mauritius na ubadilishanaji wa ndani' na 'kuelekeza sera zake katika kufikia mazingira ya fedha mazuri kwa kuimarisha shughuli ya kiuchumi na ustawi wa Mauritius.'

Benki hii imeundwa kama mamlaka iliyo na wajibu wa uundaji na utekelezaji wa sera za kifedha zilizosambamba na hali ya bei thabiti. Pia ina jukumu la kulinda utulivu na kuimarisha mfumo wa kifedha wa Mauritius.

Uuzaji wa sarafu za makumbusho kwenye Intaneti

hariri

Tarehe 12 Machi 2008, Benki Kuu ya Mauritius ilianzisha mauzo ya sarafu za makumbusho na sarafu za dahabu za Dodo kwenye intaneti kwa wanunuzi wa kimataifa. [1]

Magavana wa awali

hariri
  • Rameswurlall Basant Roi

Angalia Pia

hariri

Tazama pia

hariri
  1. "Benki Kuu ya Mauritius - Benki kuu ya Mauritius". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-08-03. Iliwekwa mnamo 2010-02-01.

Marejeo

hariri
  • Mauritius Commercial Bank. 1963. The Mauritius Commercial Bank Limited, 1838-1963. Port Louis.