Sarafu
Sarafu (kar. صرافة badilisha) ni kipande cha metali iliyotolewa na serikali ya nchi kama namna ya pesa. Mara nyingi sarafu ina umbo la duara kama kisahani. Kuna pia sarafu za pembe tatu, pembe nne au pembe zaidi.
Zamani sarafu ilikuwa umbo la kawaida ya pesa. Sarafu za kwanza zinazojulikana dunia zimepatikana kutoka Lydia katika Anatolia ya Magharibi iliyokuwa wakati ule sehemu ya utamaduni wa Wagiriki wa Kale. Sarafu zilitengenezwa hasa kwa kutumia metali ya thamani kama dhahabu na fedha, pia ya shaba na wakati mwingine ya chuma. Thamani ya sarafu ililingana na kiasi fulani cha metali hizi.
Siku hizi sehemu kubwa ya fedha inatolewa kama noti yaani kama karatasi. Karibu popote duniani sarafu hutumika kwa ajili ya pesa ndogo tu. Isipokuwa sarafu za dhahabu zinatolewa kwa idadi ndogo hasa kwa ajili ya watu wanaopenda kukusanya aina mbalimbali za sarafu zenye thamani ingawa hazitumiki kama pesa ya kulipia.
Sarafu za kihistoria
-
Tetradrachmi kutoka Athini, Ugiriki ya Kale, mnamo 480-420 KK.
-
Sarafu ya shaba iliyotolewa na Antiochus IV Epiphanes, karne ya 2 KK
-
Sarafu ya shaba kutoka nasaba ya Han nchini China, mnamo karne ya 1 KK.
-
Sestersi ya Roma ya Kale, ilitolewa na Kaisari Marcus Clodius Pupienus Maximus, 238 KK.
-
Sarafu kutoka Ufalme wa Lombardia, Italia ionyeshayo Michael Mtakatifu, mnamo 688-700 BK.
-
Dirham wa kwanza wa Ukhalifa wa Umawiyya, 729 BKD.
-
Dinari ya Almoraviya, 1138/9
-
Sarafu ya Japani mnamo 1736–1741.
-
Rupia kutoka Shirika ya East India Company, 1835