Benny Mayengani

msanii wa muziki

Bennet Skheto Baloyi (alizaliwa tarehe 11 Januari mwaka1978) akijulikana kwa jina la ukumbini kama Benny Mayengani, ni mwanamuziki kutoka nchini Afrika kusini. Alikuja kupata umaarufu baada ya kutoa albamu yake ya Tiba Ben ya mwaka 2011.

Maisha katika muziki hariri

Benny Mayengani anajulikana vizuri kutokana na ushiriki wake katika kikundi cha muziki kiitwacho Limpopo Poison ambacho kiliundwa na wanamuziki Jambatani, Prince Ranghani, Joe Shirimani na Vana va Ndoda. Aliachia albumu yake iitwayo Tiba Ben mnamo mwaka 2011 ambayo ilimpa umaarufu mkubwa na kumtambulisha katika muziki wa Xitsonga. Mnamo tarehe 28 Septemba mwaka 2013 katika kipindi cha tuzo za Xitsonga, Benny Mayengani alitunukiwa tuzo katika vipengele vitatu, kama msanii bora wakiume, nyimbo bora ya mwaka na katika album bora ya mwaka.[1]

Albumu yake ya 10 iitwayo Ni Happy ambayo iliachiwa mnamo mwaka 2019 ilishindanishwa kwenye tuzo za muziki za limpopo kwenye kipengele cha msanii bora wa kiume[2]. Benny mayengani kwasasa amatoa albamu yake iitwayo "malambani" tarehe 27 Novemba mwaka 2020 ambayo ilikuwa ikishika nafasi ya juu kabisa kwenye itune kwa kipindi cha siku nne mfululizo, hivyo unaweza kusema kuwa albamu yake hii imefanya vizuri sana katika majukwaa ya mitandaoni.

Siasa hariri

Ukiachilia maisha yake ya muziki Benny Mayingani ndiye aiyekuwa mwanamuziki wa kwanza wa Tsonga kuwa katika baraza la Johannesburg kama mwakilishi, lililo chini ya Wapiganaji wa Uhuru wa Kiuchumi mnamo mwaka 2016.[3]

Marejeo hariri

  1. "Radiobiz » Blog Archive » Xitsonga Music Awards Nominees revealed" (kwa en-US). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-03. Iliwekwa mnamo 2022-04-26. 
  2. Eyewitness News. "4 nominations for Sho Madjozi, Candy Tsamandebele for Limpopo Music Awards". ewn.co.za (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-26. 
  3. "The President of Tsonga music becomes PR Councilor for EFF in the City of Johannesburg". VIV Lifestyle Magazine (kwa en-US). 2016-08-29. Iliwekwa mnamo 2022-04-26.