Wasanii

Wasanii ni wale watu wote wanaohusika na kazi inayojumuisha sanaa, kwa mfano: wachoraji, waimbaji, wahunzi n.k.

Kazi hiyo inadai ubunifu mkubwa kuliko kawaida, unaowawezesha kutambua mambo mbalimbali na kuyatengenezea mwangwi kwa ajili ya jamii.