Kabila la Benyamini

(Elekezwa kutoka Benyamini (Israeli))

Kabila la Benyamini ni mojawapo kati ya makabila ya Israeli ambayo kwa jumla ni 12, kutokana na watoto wa kiume 12 wa Yakobo Israeli, babu yao kulingana na historia, Benyamini alipendwa sana baada ya Yusufu kupotea.

Lilipewa na Yoshua eneo katikati ya nchi, ulipokuwa mji wa Yerusalemu. Hasa baada ya kupigana na makabila mengine yote pamoja, na hatimaye kushindwa, lilibaki dogo kabisa. Hata hivyo mfalme wa kwanza wa Israeli yote, Sauli, alitokea kabila hilo.

Mtu maarufu zaidi wa kabila hilo ni Mtume Paulo.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kabila la Benyamini kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.