Bia
Bia ni kinywaji cha pombe kinachotengenezwa kwa maji, nafaka hasa shayiri, hopi kwa ladha na hamira kama chachu. Kiwango cha alikoholi ndani yake ni kati ya asilimia 2 - 6.
Bia katika Afrika ya Mashariki
haririKimsingi bia si tofauti sana na kinywaji kinachoitwa "pombe la kienyeji" kama kinatengenezwa kwa kutumia nafaka kama mahindi au mtama. Tofauti ni hasa katika chachu yaani matumizi ya hamira iliyochaguliwa hasa bafdala ya chachu asilia kutoka hewa jinsi ilivyo katika pombe la kienyeji halafu usanifishaji pamoja na kupitisha kinywaji katika filta kwa kuondoa sehemu nzitonzito ndani yake.
Viwanda vya bia vilianza kufanya biashara katika mji wa Dar es Salaam mwaka 1906 wakati wa ukoloni wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Bwana Wilhelm Schultz alikuwa mmilikaji wa biashara hii. Biashara hii iliharibiwa na Waingereza katika mwaka 1916, lakini biashara ingine ilianza kuuza bia katika mwaka wa elfu moja mia tisa ishirini na mbili nchini Kenya na Tanzania. Biashara hii mpya iliitwa “Kenya Breweries Limited.”
Mwanzoni waafrika wa mashariki hawakuruhusiwa kununua bia katika chupa. Bali kanuni ilibadilishwa baada ya sheria mpya ilipopitishwa mwaka wa 1947. “Kenya Breweries Limited” au “KBL” na “East African Breweries Limited” au “EABL” zilitawala soko la bia kwa muda mrefu kabisa.
Baada ya harakati za uhuru katika miaka ya sitini bia ilikuwa ishara ya utaifa. Mathalani, bia ya Tusker ilikuwa bia ya taifa nchini Kenya. Tusker ni bia maarufu kuliko mabia yote. Kabla mwaka wa elfu moja mia tisa sabini na saba serikali za Tanzania na Uganda zilimiliki biashara za bia, lakini biashara “KBL” ilibaki katika sekta ya binafsi nchini Kenya. Katika miaka ya tisini “Vita za bia” zilifanyika. Biashara nyinge zilipambana. Kuna biashara nyingi za bia sasa katika Afrika ya Mashariki.
Baadhi ya watu hupika pombe yao wenyewe. Wanawake hupika pombe nyumbani kwa kawaida. Ujuzi wa kupika pombe ni rahisi. Katika karne ya elfu moja na mia tisa, watu walitumia mtama na mkota kupika pombe. Mpaka sasa watu hawakutumia mahindi. Lakini siku hizi mahindi ni kiambato cha kinachopendwa sana. Ndizi hutumika kutengeneza divai. Watu wa Afrika ya Mashariki hunywa pombe na divai katika vyungu vikubwa. Pombe hutumika katika sherehe nyingi katika Afrika ya Mashariki. Unywaji ni sababu kujuana.