Mahindi ni mbegu za mmea wenye asili ya Amerika ambao unaitwa mhindi na chakula muhimu cha watu katika pande nyingi za dunia.

Masuke ya aina mbalimbali za mahindi.

Ni nafaka yenye wanga na katika Afrika ya Mashariki huliwa hasa kama ugali. Ugali unatengenezwa kwa kutumia unga wa mahindi.

Mahindi mabichi yasiyokauka huliwa pia kwa kubanika suke lote juu ya moto.

Mahindi yaliyosagwa hutumiwa pia kwa kutengeneza pombe ya kienyeji.

Utangulizi

hariri

Mhindi (jina la kisayansi: Zea mays), ni unyasi ulioanza kulimwa na watu wa Amerika tangu nyakati za kale. Watu wa Amerika walilima mahindi ya aina mbalimbali.

Tamaduni za Mississippi, jimbo ambalo mji wake mkuu na nyumbani mwa utawala wa Cahikia ambako sasa ilipo Illinois ya sasa, ulifikia kilele chake mwaka 1250, na kuwa na watu wengi na kukua kibiashara kutokana na kilimo cha mahindi.

Mfano mwingine ni wanawake wa Pawee, kwenye Nyanda za juu, walifahafamika kwa kulima aina kuu mbili za mahindi mwishoni mwa karne ya 18.

Baada ya watu wa Ulaya kufika Marekani, wafanyabiashara na wachunguzi walibeba mahindi mpaka Ulaya na kuyatambulisha kwenye nchi nyingine kupitia biashara. Matumizi yake yakaenea dunia nzima.

Mahindi ndiyo zao linalolimwa kwa wingi kuliko yote huko Amerika (tani za metriki milioni 332 kila mwaka kwa Marekani pekee). Mahindi mahuluti yanapendwa na wakulima wengi kwa sababu ya mazao yake mengi baada ya kubadilisha kizazi chake.

Wakati baadhi ya mimea ya mahindi’ ikikua hata kufikia urefu wa mita 7, yale yanayokuzwa kibiashara mengi huwa na urefu wa mita 2.5.

Mahindi aina ya Sweet corn ni fupi kuliko aina nyingine za mahindi.

Maumbile na tabia za kimaumbile

hariri

[[1]] mmea mchanga wa mahindi.

Mashina ya mahindi hufanana kwa nje na miti ya mianzi, na pingili zake zinaweza kufikia hata sm 20 – 30 kwa urefu. Mahindi hukua haraka kwa utaratibu maalumu; majani ya chini yakiwa kama bendera pana, yenye urefu wa sm 50 – 100 na upana wa sm 5 – 10; mashina husimama wima, mara nyingi mita 2 – 3, na kuwa na majani mengi yaliyomwagika kila upande. Chini ya majani haya nakaribu ya shina hukua mashuke. Hukua na kuongezeka urefu kwa milimita 3 kwa siku. Mashuke haya ni sehemu ya kike ya mmea wa mahindi, ikiwa imefungwa vizuri na majani ya kutosha, na hivyo kufunikwa kwenye shina mpaka pale itakapojitokeza ndevu za njano mwishoni mwa mashuke hayo. Mashuke hayo kimsingi ni stigima ndefu ambazo huonekana kama mrundikanao wa nywele, awali wenye rangi ya kijani lakini baadae huwa na rangi ya njano. Jamii nyingine za mahindi zimezalishwa kuzalisha mashuke mengi zaidi.

[[2]] mmea wa mahindi ukionesha mashuke, kikoyo na ndevu za mahindi. Ncha ya shina huishia kwa shada, iitwayo mbelewele, sehemu ya Ua ya kiume ya mmea wa mahindi. Kisha mbelewele kukomaana hali ikiwa kavu na yenye joto la kutosha, basi poleni kutoka sheme hiyo ya kiume ya ua huachiwa tayari kwa uchavushaji. Poleni za mahindi husafirishwa kwa upepo na huweza kusafiri mita kadhaa. Ndevu zile huweza kupokea poleni, kila shuke huzalisha muhindi. Na huweza kuliwa yakiwa mabiichi lakini kadiri muda unavyozidi kwenda nayo huzidi kuwa makavu. Na mpaka mwisho wa msimu wa mavuno huwa ni vigumu kabisa kutafuna na huhitaji kwanza kulainishwa kwa kuchemshwa. Namna bora za kilimo hupenda kuzalisha muhindi mmoja kwa kila mmea ili kupata wenye ukubwa mzuri na wenye kufaa.

Mbegu za mahindi huwa na sehemu ya nje iliyoungana na gamba la nje la mbegu, kama ilivyo kawaida kwa mimea mingi ya jamii ya nyasi. Muhindi huwa na mbegu nyingi, ambazo huwa haziungani hata maramoja , na kila moja ikiwa na ukubwa wa kama Njegere hivi, zikiwa zimejipanga kwenye mistari kuzunguka gunzi ambamo zimejishikiza. Gunzi moja huweza kuwa na punje za mahindi takribani 200 – 400, na huwa na urefu wa sentimita 10 -25. Pia huwa na rangi mbalimbali: nyeusi, kijivu, nyekundu, Hudhurungi, nyeupe na njano. Zinaposagwa kuwa unga, unga wa mahindi hupatikana kwa kiasi kikubwa, huku ukiwa na makapi kidogo kuliko Ngano. Lakini unga wa mahindi huwa unakosa protini muhimu ya ngano, na hivyo, kufanya uokaji kushindwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuumuka na kufanana.

Kiwango cha uzalishaji na mbinu.

hariri

[[3]]] kiwango cha uzalishaji wa mahindiduniani 2005

[[4]] uvunaji wa mahindi wakati wa uvunaji wa rekodi huko Jones County, Iowa, mnamo 2009

Mahindi yanalimwa duniani kote, na uzito wa mahindi huzalishwa kila mwaka zaidi ya mwaka uliopita. Wakati Marekani ikizalisha karibu nusu ya mahindi yote duniani, ( ~42.5%), nchi nyingine zinazoafanya vizuri ni China, Brazil,Mexiko, Argentina, Uhindi na Ufaransa. Uzalishaji wa dunia ni karibu tani milioni 800 mwaka 2007, juu kidogo tu ya mchele ( tani milioni 650) na ngano ( ~tani milioni 600). Mwaka 2007, zaidi ya hekta milioni 150 za mahinid zilipandwa dunia nzima, kwa zaidi ya kg 4970.9 kwa hekta. Mazao yanaweza kuwa zaidi ya hapa kwa baadhi ya maeneo mengine duniani; utabiri wa mwaka 2009 unaonesha Iowa ingezalisha kg 11614 kwa hekta.

Matumizi

hariri
 
mahindi yakivunwa kwa namna ya asili

Kama chakula

hariri

Mahindi hutumika kama chakula kikuu kwa maeneo mengi duniani. Mlo wa mahindi huliwa kama uji mzito (mfano Tanzania na Nchi nyingi wa Afrika ya Mashariki huita “ugali”), katika tamaduni nyingi: kuanzia huko Italia kama poleta, Brazili kama angu, Romania kama mamaliga mpaka mush huko Marekani au sadza, nshima, ugali na mealie pap katika Afrika. Mlo wa mahindi pia hutumika badala ya unga wa ngano, kutengeneza baadhi ya aina ya mikate na vyakula vingine vya kuoka. bisi ni mahindi ya pekee ambayo hupasuka na kufanyiza chakula kitamu ambacho huliwa kama chakula cha kutafuna. Pia mahindi yakiwa bado laini kidogo yaweza kuchomwa na kuliwa tena kwa kutafuna, na huweza kuongezwa ladha kwa kutia chumvi, pilipili au viungo vingine. Hicho ni baadhi ya chakula maarufu huko Vietnam. Chicha na “chicha morada” ni baadhi ya vinywaji maarufu vinavyotengenezwa kwa aina fulani ya mahindi. Hicho cha kwanza huchachushwa na huwa na kilevi, huku cha pili ni kinywaji baridi na hunywewa sana huko Peru.

 
mahindi aina ya Sweet White Corn

mahindi pia yana weza kutumiwa yakiwa hayajaiva, wakati yamekomaa lakini bado ni laini. Katika hali hii huweza kuchemshwa ili kuwa na ladha nzuri, na kula punje zake kutoka kwenye gunzi. Wakati mwingine mbegu hizo kisha kuchemshwa hupukuchuliwa na kuchanganywa na mboga majani nyingine kama vile saladi wakati wa kuandaa chakula. Pia huweza kupikwa na vykula vingine kutoa mchanganyiko wa makande, purée, tamales, pamonhas, curau, keki, n.k. mahindi aina ya Sweet Corn huwa na ladha nzuri sababu ya kiasikikubwa cha sukari na wanga mpaka kuweza kuliwa yakiwa katika hali ya ubichi.

[[5]] = mchuuzi wa mahindi ya kuchoma huko India.

Kiwango cha virutubisho vya mahindi Carbohydrates 19.02 g Sugars 3.22 g Dietary fiber 2.7 g Fat 1.18 g Protein 3.22 g Tryptophan 0.023 g Threonine 0.129 g Isoleucine 0.129 g Leucine 0.348 g Lysine 0.137 g Methionine 0.067 g Cystine 0.026 g Phenylalanine 0.150 g Tyrosine 0.123 g Valine 0.185 g Arginine 0.131 g Histidine 0.089 g Alanine 0.295 g Aspartic acid 0.244 g Glutamic acid 0.636 g Glycine 0.127 g Proline 0.292 g Serine 0.153 g Water 75.96 g Vitamin A equiv. 9 µg (1%) - lutein and zeaxanthin 644 µg Thiamine (Vit. B1) 0.200 mg (15%) Niacin (Vit. B3) 1.700 mg (11%) Folate (Vit. B9) 46 µg (12%) Vitamin C 6.8 mg (11%) Iron 0.52 mg (4%) Magnesium 37 mg (10% Potassium 270 mg (6%)

Huko Marekani na Kanada mahindi hutumiwa sana kwaajili ya chakula cha mifugo, au mbegu. Mlo wa mahindi pia ni viungo vya chakula maalumu cha mazao ya wanyama kama vile, hot dog. Mahindi pia hutumika huko ulaya kama chambo cha kuvulia samaki. Kemikali na madawa.

Wanga unaopatikana kwenye mahindi unaweza kutumika kutengeneza plastiki, madawa na bidhaa nyingine za kikemikali.

Stigima kutoka kwenye sehemu ya kike ya ua la mmea wa mahindi huuzwa kama dawa.

Utengenezaji wa fueli

hariri

Mahindi pia hutumika kutengenezea fueli kutoka kwenye mabaki yake ya mimea. Magunzi yake pia hutumika kama chanzo cha nishati. Mahindi hupatikana kwa urahisi, na kufanya upatikanaji wa nishati hiyo nyumbani kuwa rahisi zaidi.

  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mahindi kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.