Bill Clinton


William Jefferson Clinton (alizaliwa tar. 19 Agosti 1946), anafahamika zaidi kama Bill Clinton, alikuwa rais wa 42 wa Marekani. Alianza kutumikia taifa la Marekani kuanzia mwaka wa 1993 hadi 2001. Alipochaguliwa kuwa rais, alikuwa na umri wa mika 46. Mpinzani wake mkubwa alikuwa mzee George H. W. Bush na Bw. Bob Dole.

Bill Clinton


Rais wa Marekani
Aliingia ofisini 
January 20, 1993
Makamu wa Rais Al Gore
mtangulizi George H. W. Bush
aliyemfuata George W. Bush

tarehe ya kuzaliwa 19 Agosti 1946 (1946-08-19) (umri 77)
chama Democratic
ndoa Hillary Clinton
watoto Chelsea Clinton
makazi New York
mhitimu wa Georgetown University
signature

Clinton alikuwa rais wa kwanza kutoka kizazi cha Baby Boom na alikuwa rais wa tatu kijana kutumikia taifa la Marekani. Clinton anatokea chama cha Kidemokrasia. Wasaidizi wa Clinton wanasema ya kwamba rais huyo alisaidia kuinua uchumi wa Marekani katika miaka ya 1990. Wakati urais wake, kulikuwa na mijadala mikali kati yake na chama chake cha Wana-Demokrasia dhidi ya wanasiasa wa chama cha Republicans. Kabla ya kuwa rais, Clinton alikuwa gavana wa jimbo la Arkansas kuanzia mwaka 1979 hadi 1981, na vilevile mwaka 1983 hadi 1993 .

Mnamo mwaka 1994, wakati wa kipindi cha kwanza cha uraisi wa Clinton, Bunge la Marekani, lilikuwa linamilikiwa na Wana-Republican. Hata hivyo, Clinton aliendelea kumshinda mmoja wa wagombea Urais kutoka chama cha Republicans Bw. Bob Dole, katika uchaguzi uliofanyika mwaka wa 1996 .

Rais Clinton alishtakiwa na Seneti ya Marekani mnamo mwezi Disemba 1998 kwa kashfa za kusema uwongo mbele ya mahakama kuhusu mahusiano ya kimapenzi na Bi. Monica Lewinsky.

Kashfa hii ilimshushia hadhi yake kidogo.Hata hivyo alikuwa rais aliyekubaliwa na raia wengi hadi mwisho wa kipindi chake. Alipoacha ikulu bajeti ya nchi ilikuwa na ziada ya pesa kwa mara kwanza tangu miaka ya 40.

Rais Clinton na Pele wakicheza mpira

Bill, amemwoa Seneta Hillary Clinton na kwa sasa wanaishi mjini New York.

Tazamia pia

hariri

Viungo vya Nje

hariri

}}