Binti (filamu ya 2021)
Binti ni filamu ya kuigiza ya Tanzania ya mwaka 2021 iliyoongozwa na Seko Shamte na kutayarishwa na mkurugenzi mwenyewe na Alinda Ruhinda na Angela Ruhinda.
Waigizaji nyota wa filamu hii ni Bertha Robert, Magdalena Munisi, Helen Hartmann na Godliver Gordian katika nafasi kuu huku Yann Sow, Alex Temu na Jonas Mugabe wamecheza nafasi za wasaidizi[1].
Filamu hii inahusu hali ya wanawake wa kisasa jijini Dar es Salaam katika sura nne: Tumaini, Angel, Stella na Rose.
Filamu hiyo imerekodiwa ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam, Tanzania. Marekebisho ya rangi yalifanyika India na jiji la Los Angeles, na sauti ilifanyika Misri.
Onyesho la kwanza la filamu hii lilicheleweshwa kwa miaka miwili kwa sababu ya janga la UVIKO-19.[2]
Filamu hii ni ya kwanza ya Kitanzania kuonyeshwa Netflix[3].
Waigizaji
hariri- Bertha Robert kama Tumaini
- Magdalena Munisi kama Angel
- Helen Hartmann kama Stella
- Godliver Gordian kama Rose
- Yann Sow kama Emma
- Alex Temu kama Ben
- Jonas Mugabe kama James
- Hadija Athumani Saidi kama Tumaini mdogo
- Hasham H. Hasham kama Sonara
- Jaffari Makatu kama Baba yake Tumaini mdogo
- Levison Kulwa James kama Pacha wa kwanza
- James Doto James kama Pacha wa pili
- Betty Kazimbaya kama Mama Tumaini
- Akbar Thabiti kama Nelson
- Tiko Hassan kama Tamala
- Tamala S. Kateka kama Dereva wa gari la kutorokea
- Francis Mpunga kama Baba Tumaini Mzee
- Anatoly Shmakor kama Polisi wa Ulaya
- Suleiman Mchora kama Polisi
- Neema Wlele kama Catherine
- Angel Henry George kama Alinda
- Jane Masha kama Doris
- Yasser Msellem kama Omari
- Sauda Simba Kilumanga kama Mama Angel
- Rita Paulsen kama Daktari Ruhinda
- Hailath Maiko kama Msaidizi wa Stella
- Patricia David kama Mhudumu
- Kyan Ishau kama Chris
- Ruqahya Ramadhani kama Irene
- Abubakar Amri kama msaidizi Rose
- Chiku Seif kama Fatima
- Regina Kihwewle kama Mwalimu wa shule
- Izack Lukindo kama Daktari Shamte
- Abdallah Minyuma kama Fundi wa Kompyuta
- Kiswiju Mpyanga kama Mama Rose
Marejeo
hariri- ↑ Musisi, Nakanyike B. (2021), "Women in Pre-colonial Africa: East Africa", The Palgrave Handbook of African Women's Studies, Springer International Publishing, ku. 1073–1097, iliwekwa mnamo 2022-08-06
- ↑ "'Binti': Film by women, about women". The East African (kwa Kiingereza). 2021-03-26. Iliwekwa mnamo 2023-05-14.
- ↑ "Tanzania Scores its First Netflix Film Release with 'Binti.' - OkayAfrica". www.okayafrica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-05-14.
Viungo vya nje
hariri- Binti kwenye IMDb
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Binti (filamu ya 2021) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |