Bishkek (Bichkiek) ni mji mkuu wa Kirgizia. Ina wakazi 900,000 (2005).

Muonekano wa Mji wa Bishkek


Jiji la Bishkek
Nchi Kirgizia

Historia hariri

Mji ulianzishwa kama kituo cha misafara kwenye barabara ya hariri kati ya China na Mashariki ya Kati. Khan wa Kokand alitengeneza hapa boma lililotwaliwa na jeshi la Urusi 1862 wakati wa uenezaji wa Urusi katika Asia ya Kati.

1878 Warusi walijenga mahali palepale kituo cha kijeshi kwa jina la "Pishpek" (Пишпек). Kituo kikakua haraka kuwa mji kwa sababu wakulima Warusi walipewa mashamba katika eneo hili.

Baada ya mapinduzi ya Urusi ya 1917 mji ulibadilishwa jina ukaitwa "Frunze" (Frunzie) kwa heshima ya jemadari mkomunisti Mikhail Frunze.

Tangu kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti mwaka 1991 mji ukawa mji mkuu wa nchi mpya ya Kirgizia ikarudishwa jina la kale kwa umbo la "Bishkek".

 
Barafuto ya Ala-Archa karibu na Bishkek
  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bishkek kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.