Uwanja wa michezo Borg El Arab
Uwanja wa Borg El Arab, mara nyingine hufahamika pia kama Uwanja wa Jeshi la Misri au Uwanja wa El Geish- Alexandria, ni uwanja uliozinduliwa mwaka 2005 katika hoteli ya Mediterranean ambayo ni sehemu yaBorg El Arab; tarkibani kilometa 25 magharibi mwa mji wa Alexandria, Misri. Uwanja huu ndio mkubwa zaidi nchini Misri na ni wa pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya uwanja wa FNB wa jijini Johannesburg), ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 86,000[1] na wote wakiwa wamekaa katika viti. Pia ni uwanja wa 27 kwa ukubwa duniani kwote. Uwanja huu upo jijini Cairo katika eneo la makutano ya barabara ndani ya jangwa la Alexandria takribani kilometa 10 kutoka uwanja wa ndege wa Borg El Arab na kilometa 15 kutoka katikati ya mji wa Alexandria. Kuna njia kwa ajili ya michezo ya mbio kuzunguka eneo la kuchezea la uwanja huo, na kuna minara ya taa katika kila pembe ya uwanja. Jukwaa moja pekee ndilo lililoezekwa.
Uwanja mzima una ukubwa wa mita za mraba 609,000 na kuna ukuta uliozunguka wenye urefu wa kilometa 3 na miundombinu ya barabara yenye urefu wa kilometa 6, eneo la kuegesha magari lenye uwezo wa kuingiza magari 5000 na mabasi 200 kuachana na eneo maalumu kwa ajili ya ndege, pia kuna mageti 136 ya kuingilia. Jukwaa kuu limefunikwa na mwamvuli ambao umefunika tarkibani 35% ya uwanja wote, na ndio mwamvuli mkubwa kuliko yote katika mashariki ya kati. Una urefu wa mita 200 na upana wa mita 60 na eneo la mita za mraba 12,000.
Uwanja huo una mfumo wa hewa katika vyumba vya kubadilishia nguo, saluni na maeneo ya kuingilia, uwanja huo pia una mashine za kupandisha watangazaji na watu muhimu katika majukwaa ya juu ya uwanja. Kuna viwanja viwili vya mazoezi ambavyo vina uwezo wa kuingiza watazamaji 2000, vyumba viwili vya kubadili nguo na eneo kwa ajili ya michezo ya riadha. Uwanja huo una hoteli yenye uwezo wa kuingiza wageni 200 yenye mfumo wa usambazaji hewa pamoja na bwawa la kuogelea, eneo la kufanyia mazoezi na nyumba za idara zenye watu 80. Uwanja huu pia una jengo la mikutano na waandishi wa Habari. Ikijumuisha maeneo ya warusha Habari, viingilio vya dharura, magari ya huduma ya kwanza, maeneo ya kujipatia chakula 39, vyumba vya kujisaidia 337 vinavyojumuisha vyumba 33 kwa ajili ya wanawake na 8 kwa wasiojiweza.
Historia
haririWasifu
haririUwanja huu ulijengwa ikiwa ni sehemu ya viwanja 5 kujengwa katika harakati za kuwania nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010.[2] Baada ya kushindwa kupata nafasi hiyo, uwanja huu ulifanywa kuwa uwanja wa timu ya taifa ya Misri pamoja na uwanja wa michezo wa Cairo. Pamoja na timu ya taifa, klabu ya mji wa Alexandria Smouha SC ulianza kutumia uwanja huu wa michezo yake ya nyumbani badala ya Uwanja wa michezo wa Alexandria kuanzia mwaka 2016; ambapo na timu za Al Ahly SC, Al Ittihad, Al-Masry SC na Zamalek SC zimekua zikitumia uwanja huu kwa michezo yake ya nyumbani kutokana na sababu mbalimbali.
Uwanja huu una wasifu wa kipekee kwani umebuniwa na kujengwa na jeshi la Misri kuanzia mwanzo mpaka kumalizika.
Kufunguliwa
haririIli kutumia uwanja huu, Misri iliupendekeza kuwa miongoni mwa viwanja vitakavyotumika katika fainali za kombe la vijana kwa umri mwa chini ya miaka 20. Katika ukaguzi kuhakikisha Misri ipo sawa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, Bwana Jack Warner naibu raisi wa shirikisho la FIFA na mkuu wa ukaguzi aliusifu sana uwanja huu. Alisema “ Ni uwanja bora sana, ni miongoni mwa viwanja bora kabisa duniani".[3] Wajmbe wengine wa kamati hiyo ya ukaguzi walielezea uwanja huu kuwa na mfanano san ana uwanja wa Stade de France. Uwanja huu hana hivyo ulitumika katika mchezo mmoja pekee katika mashindano hayo, ambao ulikua mchezo wa ufunguzi baina ya wenyeji Misri na timu ya vijana ya Trinidad and Tobago hii ikijumuisha sherehe za ufunguzi wa mashindano.[4] Raisi wa FIFA bwana Sepp Blatter alielezea furaha yake ya kuwa katika uwnja mashuhuri wa Borg El Arab alipoweza kuona maonyesho ya taa wakati wa sherehe za ufunguzi wa mashindano.[5]
Maelezo
haririMahali
haririEneo la Borg El Arab lilichaguiwa kuwa mahali pa ujenzi wa uwanja huu. Borg El Arab ni eneo lililopo umbali wa kilometa 7 kutoka makutano ya barabara ya jangwani yeye urefu wa kilometa 31 ya Cairo-Alexandria. Pia kuna umbali wa kilometa 1o kutoka uwanja wa ndege wa Borg El Arab Airport, hosipitali ya dharura ya Mubarak na Kijiji cha kitalii katika fukwe ya kasakazini. Eneo hili pia lipo umbali wa kilometa 1.5 kutoka kituo cha treni cha king Mariot. Hoteli ya Borg El Arab inafahamika kwa usafi wake kutokana na kuwa katika eneo lenye muinuko wa mita 28 kutoka usawa wa bahari.
Eneo lililopendekezwa kwa ujezi wa mradi huu lina ukubwa wa mita za mraba 600,000 sawa na hekari 145 na uligawanywa kama ifuatavyo: 30% kwa ajili ya majego, 30% kwa ajili ya barabara na maeneo ya mapumziko, 40% mioto. Mradi huu unategemewa kuwa ujenzi kwa matofli wa eneo kama Kijiji cha michezo.
Viingilio na Kutoka
haririUkuta wenye urefu wa kilometa 3.5 unazunguk uwanja huu. Kuna malango 10 na maduka 80 kwa ujumla ikiwa nae neo la mita za mraba 4000. Uwanja mkuu umezungukwa na uzio wenye urefu wa kilometa 1.2 kwa ajili ya kuzuia watazamaji. Uzio huu una malango 17 na jumla ya maeneo ya kuingi 136 zenye uwezo wa kupitisha watu 800 kwa dakika moja. Wakati kjaza uwanja huu inachukua masaa mawili, kuondoa watu huchukua dakika nane pekee.
Baada ya malango ya kuingilia, kuna safu za ngazi 76, zikigawanyika 22 kuelekea majukwaa ya juu, 18 kuelekea chini katika vyumba maalumu, 36 chini katika majukwaa ya chini. Viingilio vingine ni kwa ajili ya watu muhimu, wasiojiweza na watu wenye mahitaji maalumu. Uwanja huu pi una lifti 8, 2 kwa ajili ya watu muhimu, 2 kwa ajili ya waandishi wa Habari, 2 kwa ajili ya bidhaa na vifaa na 2 kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalumu.
Uwanja huu una viingilio kama ifuatavyo, moja kuelekea eneo la kucheza, moja kwa ajili ya riadha, mbili kwa ajili ya magari ya hudumua ya kwanza na zima moto, moja kwa ajili ya wachezaji na wahudumu. Na mbili kwa ajili ya vikundi vya mashabiki.
Kiwanja
haririMuelekeo wa kijografia wa kiwanja cha kucheza ni nyuzi 12 kaskazini magharibi ili kuendana na uelekeo wa upepo. Sababu kuu ikiwa ni kuepuka kuzuiwa kwa mpira au mchezaji kulingana na sheria za FIFA. Vipimo vya uwanja ni mita 105 * 70. Kuachana na kiwanja, uwanja huu una eneo la kuendesha mashindano ya Olimpic, sehemu 8 wa ajili ya michezo ya kukimbia, sehemu mbili zenye mchanga kwa ajiliya kuruka umbali mrefu na sehemu moja ya mchanga kwa ajili ya mchezo wa kuruka mara tatu.
Kiwanja kina minara ya taa miwili, upande wa kaskazini sharaki na kusini mashariki na zina urefu wa mita 65 kutoka chini. Pamoja na hayo, mfumo wa mwanga umewekwa katika vivuli vya jua. Skrini mbili za kuonyesha matokeo pamoja na maeneo 13 maalumu kwa ajili ya kuweka kamera.
Na pia kuna viwanja viwili kwa ajili ya mazoezi vyenye uwezo wa kuingiza watazamaji 2000 kila kimoja. Kila kiwanja kimechukua eneo la mita za mraba 3,000, ambapo kila kiwanja kina eneo la riadha, vyumba viwili wa kubadili nguo kwa ajili ya wachezaji, vyumba viwili vya kubadili nguo kwa ajili ya waamuzi, ofisi na vyumba vya kupumzikia. Viwanja vyote hivi vina Minara ya taa pia.
Uwezo wa Mashabiki
haririMajukwaa makubwa ya uwanja wa Borg El Arab yana uwezo wa kubeba mashabiki 86,000 katika ngazi za juu na chini. Kwa jinsi jukwaa zilivyojengwa, inamuwezesha mshabiki kuone sehemu yoyote ile ya kiwanja bila ya kuzuiwa na kitu chochote. Wakati chumba cha watu muhimu kina viti 22 tu, eneo hilo lina uwezzo wa kuingiza watazamaji 300. Eneo la waandishi wa Habari lina uwezo wa kuingiza watu 300. Jukwaa la je pia lipo kwa mashabiki wenye mahitaji muhimu.
Eneo la kusimama pamoja na eneo daraja la kwanza ambazo kwa pamoja huwakilisha 35% ya eneo zima la washabiki, limefunikwa nap aa la kuzuia jua lenye urefu wa mita 200 na upana wa mita 62. Paa hilo limeshikiliwa urefu wa mita 32 kwa nguzo 18 zenye maumbo ya maua.
Huduma zinazopatikana
haririVyumba vinne vya kubadilisha nguo, na vyumba vya kupumzika na kuoga vimejumuishwa katika kila moja, vinapatikana kwa wachezaji. Kwa kuongezea, vyumba viwili vya joto, idadi ya ofisi za makocha na wafanyikazi wa matibabu, vyumba kadhaa vya waamuzi, kumbi za michezo, kituo cha matibabu kilicho na maabara ya uchambuzi wa kiwango cha juu zaidi, na kituo cha waandishi wa habari cha habari.
Kwa watazamaji, kuna migahawa 32 na vyumba vya kupumzika 68 (jumla ya vyoo 386; 337 kwa wanaume, 43 kwa wanawake, na 6 kwa watu wenye mahitaji maalum). Asilimia ishirini na tano ya uwanja huo ina kiyoyozi, hii ni pamoja na mtaro, saluni, vyumba vya kubadilishia nguo, na kituo cha media. Kamera za sauti na ufuatiliaji zinapatikana kwenye chumba cha kudhibiti kinachopatikana kwenye basement. Mtandao wa usafirishaji wa habari na mtandao wa kengele za moto zimeunganishwa na chumba cha kudhibiti kati kilichopatikana sehemu ya juu ya uwanja.
Uwanja huo unajumuisha hoteli ya wachezaji ambayo inajumuisha kitanda 200 ambacho kina viyoyozi. Hoteli hiyo inajumuisha ukumbi wa mikutano, mkahawa, mgahawa, bwawa la kuogelea, ukumbi wa mazoezi na mtoaji wa lifti. Mbali na hoteli hiyo, pia kuna jengo la kiutawala na kituo cha makazi cha wafanyikazi wa uwanja huo chenye uwezo wa jumla ya watu 80 (jumla ya eneo ni mita za mraba 3500). Jengo hili linajumuisha ofisi kadhaa, salons, ukumbi wa kulia, malazi ya vyumba. Uwanja huo unajumuisha mtandao wa barabara wa ndani ambao una urefu wa kilomita 6 & nbsp;, maegesho ya gari ya magari elfu 5, na mabasi 200 na pedi ya kutua helikopta yenye uwezo wa ndege 4.
Sehemu za kijani za tovuti zinachukua jumla ya mita za mraba 250,000. Tovuti imekuwa malisho 4 Mb ya umeme, jenereta mbadala ya umeme, laini 500 za simu za mitaa, laini za simu za kimataifa za 1500, tanki la maji la ardhini lenye uwezo wa mita za mraba 2000, na rasimu ya uwezo wa maji taka 800 m.
Marejeo
hariri- ↑ "The boys are ready", Al-Ahram Weekly, na. 965, Al Ahram Publishing House, 17 Septemba 2009, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Oktoba 2010, iliwekwa mnamo 6 Juni 2010
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "The stadiums and their cities" Archived Oktoba 31, 2010, at the Wayback Machine. Al Ahram Weekly, 2003-12-31. Retrieved on 10 June 2010.
- ↑ Mazhar, Inas "Test tour" Archived Oktoba 11, 2010, at the Wayback Machine. Al Ahram Weekly, 2008-03-19. Retrieved on 10 June 2010.
- ↑ Pugmire, Jerome (25 Septemba 2009), "Blatter kicks Maradona while he's down and says Argentina in 'crisis'", The Scotsman, Johnston Press, iliwekwa mnamo 6 Juni 2010
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Egypt welcomes the world" Ilihifadhiwa 5 Machi 2016 kwenye Wayback Machine. FIFA, 2009-9-24. Retrieved on 10 June 2010.