Mchezo wa ngumi

(Elekezwa kutoka Boxing)

Mchezo wa ngumi ni aina ya michezo ya mapigano ambapo mabondia wawili wanapigana kwa kutumia ngumi pekee kwa kufuata kanuni za mchezo. Wote wawili huvaa glavu nene kwa shabaha ya kupunguza hasara za kiafya.

Mchezo wa ngumi
Vijana wa Ugiriki ya Kale wakipigana kwa ngumi

Mashindano yasimamiwa na refa, kwa kawaida mbele ya watazamaji na kutekelezwa ndani ya mzingo maalumu.

Mashindano yamegawiwa kwa vipindi vinavyodumu dakika 1 - 3. Shabaha ni ama kumpiga mshindani hadi asiweze kuendelea tena au kufikisha mapigo mengi kichwani na tumboni yatakayohesabiwa na refa na kuamulisha ushindi.

Historia

Watu waliwahi kupigana kwa kutumia ngumi kwa kufuata kanuni fulani tangu milenia nyingi.

Mchezo wa ngumi jinsi ulivyoenea leo kote duniani ulianza Uingereza katika karne ya 19.