Brandon Auret

Muigizaji wa Afrika Kusini

Brandon Auret (alizaliwa Disemba 27 1972) ni mwigizaji wa Afrika Kusini anayefahamika kama Leon du Plessis kwenye tamthiliya ya Isidingo.

Maisha ya mwanzoEdit

Auret amezaliwa Desemba 27 1972 katika mji wa Johannesburg huko Afrika Kusini. Kwa sasa anaishi Gauteng, Afrika Kusini.

Kazi ya UigizajiEdit

Auret alicheza kama Leon du Plessis kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2005. Baada ya kuachana na tamthiliya hii aliigiza katika safu ya kuigiza ya GO / M-Net ya Angel's Song kama William. Jukumu hili lilikuwa kuanzia 2006 hadi 2007. Sifa zingine za uigizaji wa runinga ni pamoja na: Zet, Egoli, SOS, Laugh Out Loud, One Way, Wild At Heart na Tshisa.[1] Auret ameigiza kwenye filamu ya kiafrika kusini inayofahamika kama District 9.[2]


Auret ni mmiliki mwenza na mtayarishaji wa media ya utangazaji na kampuni ya utengenezaji wa filamu A Breed Apart Pictures.[3]

MarejeoEdit

  1. TVSA Brandon Auret. Iliwekwa mnamo 20 October 2014.
  2. Feature Interview: Brandon Auret. Something Wicked and Inkless Media. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-10-20. Iliwekwa mnamo 20 October 2014.
  3. Who's Who Southern Africa. whoswho.co.za. Iliwekwa mnamo 20 October 2014.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Brandon Auret kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.