Brian Acton (alizaliwa mnamo 1972) ni muundaji wa programu za kompyuta wa nchini Marekani na mjasiriamali wa mtandao .[1], Pia anahudumu kama mkurugenzi mtendaji wa muda wa mtandao wa Signal Messenger LLC.[2]

Hapo awali alikuwa ameajiriwa na Yahoo!, na kuanzisha kwa pamoja WhatsApp,[3] programu ya kutuma ujumbe kwa simu ambayo ilinunuliwa na Facebook mnamo Februari 2014 kwa dola za Marekani bilioni 19, na Jan Koum. Acton aliondoka WhatsApp mnamo Septemba 2017 na kuanzisha shirika la Signal.[4] Kulingana na gazeti la Forbes (2020), Acton ndiye tajiri wa 836 zaidi duniani, akiwa na utajiri wa dola bilioni 2.5.[3]


Marejeo hariri

  1. Marlinspike, Moxie; Acton, Brian (21 February 2018). "Signal Foundation". Signal.org. Iliwekwa mnamo 21 February 2018.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. Marlinspike, Moxie (10 January 2022). "New Year, New CEO". signal.org. Signal Foundation. Iliwekwa mnamo 10 January 2022.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. 3.0 3.1 "Brian Acton". Forbes (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-08-18. 
  4. CNBC. "WhatsApp co-founder Brian Acton to leave company", CNBC, 2017-09-13. 
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Brian Acton kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.