Zeno Andrew Lucas (jina maarufu: Brother Zeno; 28 Juni 194627 Juni 2017) alikuwa mwanamuziki wa muziki wa dansi kutoka nchini Tanzania.

Brother Zeno
Jina la kuzaliwa Zeno Andrea Lucas
Amezaliwa (1946-06-28)Juni 28, 1946
Tanzania
Amekufa Juni 27, 2017 (umri 70)
Tanzania
Aina ya muziki Muziki wa dansi
Kazi yake mwimbaji/mtunzi wa nyimbo, mwanamuziki, mchambuzi wa muziki
Ala Sauti, gitaa
Miaka ya kazi Miaka ya 1970 - kifo

Brother Zeno, vilevile alikuwa mchambuzi wa muziki wa charanga. Zeno huhesabiwa kuwa miongoni mwa waanzilishi wa bendi ya Dar es Salaam Jazz Band B (maana zilikuwa A na B), bendi iliyokuwa ikiongozwa na Patrick Balisidya, ambayo ilionesha mafanikio yake kwa kasi na kuanza kuonekana kama tishio kwa Dar es Salaam Jazz Band A, chini ya Michael Enoch, bendi ikavunjwa na wanamuziki wengine wakaingizwa Dar Jazz A, lakini Patrick alienda zake na kuanzisha Afro 70 na kufanya mambo makubwa katika muziki wa dansi nchini Tanzania.

Mbeleni, Brother Zeno akajiunga na Shirika la Bima ya Taifa, yeye ndiye aliyetoa wazo la kuanzishwa kwa bendi katika shirika hilo, Bima Jazz Band na hivyo pia kupewa kazi ya kutafuta wanamuziki wa kujiunga na bendi hiyo na yeye mwenyewe kuwa kati ya wanamuziki waanzilishi wa kundi hilo lililokuja kujizolea umaarufu mkubwa.

Kwa upande wa uchambuzi, enzi hizo akishirikiana na "Mzee wa Macharanga" Charles Hillary wakati huo Radio One, alikuwa na ufahamu mkubwa wa muziki wa kutoka Cuba na hivyo kuwa mpenzi mkubwa wa watu waliopenda muziki huo.

Zeno alifariki tarehe 27 Juni, 2017 katika hospitali ya Temeke alipokuwa anauguzwa tatizo la moyo ambalo lilikuwa likimsumbua kwa takriban mwaka mmoja.[1][2]

Marejeo

hariri
  1. Kifo cha Zenno katika blogu ya Soma Latest.
  2. HATIMAE MWANAMUZIKI MKONGWE BROTHER ZENNO AZIKWA mazishi ya Zeno katika blogu ya Tanzania Rhumba.


  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Brother Zeno kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.