Buhen (Kigiriki: Βοὥν Bohón)[1] yalikua ni makazi ya kale ya Misri yaliokuepo kwenye ukingo wa Magharibi wa Mto Nile chini (Kaskazini mwa) Maporomoko makubwa ya pili ya maji katika eneo ambalo sasa ni Jimbo la Kaskazini, Sudan.

Kwa sasa imezama katika Ziwa Nasser, Sudan.  Kwenye ukingo wa Mashariki, ng'ambo ya mto, kulikuwa na makazi mengine ya kale, ambapo mji wa Wadi Halfa upo sasa . Kutajwa kwa mwanzo zaidi kwa Buhen kunatokana na stelae kwa utawala wa Senusret I.[2]  Buhen pia ni makazi ya mwanzo ya Wamisri kujulikana katika ardhi ya Nubia [3]

Marejeo

hariri