Wadi Halfa
Wadi Halfa (Kar: وادي حلفا) ni mji wa Sudan ya kaskazini kwenye mwambao wa Ziwa Nasser. Ni mwisho wa reli kutoka Khartoum na bandari ya feri kwenda Aswan nchini Misri.
Mji huu ulianzishwa katika karne ya 19. Baada ya 1976 wakati wa kumaliza lambo la Aswan palikuwa na mipango ya kuubomoa na kuuacha mji kabisa. Serikali ilihamisha wakazi kwenda "Halfa mpya" mji mpya mbali upande wa kusini. Lakini sehemu ya wakazi waliobaki wakakataa kuondoka wakaanza kujenga nyumba mpya jirani na nyumba zilizoanza kuzama wakati maji ya Ziwa Nasser yalipofurika.
Siku hizi Wadi Halfa imekuwa kituo muhimu cha mawasiliano kati ya Misri na Sudan.
Mji una wakazi 15,000.
Makala hii kuhusu maeneo ya Sudan bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wadi Halfa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |