Ziwa la Nasser
Ziwa la Nasser (kwa Kiarabu بحيرة ناصر, buhairat nāssir) ni bwawa kubwa kwenye mto Nile lililopatikana tangu kufungwa kwa mwendo wa Nile kwa lambo la Aswan nchini Misri kuanzia mwaka 1958.
Lake Nasser | |
---|---|
Ramani inayoonyesha eneo la ziwa | |
Anwani ya kijiografia | 22°25′N 31°45′E / 22.417°N 31.750°E |
Aina ya ziwa | Kiegezo |
Mito ya kuingia | Nile |
Mito ya kutoka | Nile |
Nchi za beseni | Egypt, Sudan |
Urefu | km 550 (mi 340) |
Upana | km 35 (mi 22) |
Eneo la maji | km2 5 250 (sq mi 2 030) |
Kina cha wastani | m 25.2 (ft 83) |
Kina kikubwa | m 180 (ft 590) |
Mjao | km3 132 ([convert: unit mismatch])[1] |
Urefu wa pwani (km) | km 7 844 (ft 25 735 000) |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB | m 183 (ft 600) |
Marejeo | [1] |
1 Shore urefu is not a well-defined measure. |
Ziwa Nasser liko katika eneo la nchi za Misri na Sudan, hasa kati ya miji ya Aswan (Misri) na Wadi Halfa (Sudan). Eneo lake ni zaidi ya km² 5,200, lina urefu wa kilomita 550 na upana hadi km 35. Mjao hufikia hadi km³ 160.
Jina lilitolewa kwa heshima ya aliyekuwa rais wa Misri Gamal Abdel Nasser aliyefanya azimio la kujenga bwawa.
Faida na matatizo ya ziwa
haririKuzuiliwa kwa mwendo wa mto ulimaliza mafuriko ya kila mwaka ya Nile nchini Misri. Kwan upande mwingine matope yenye rutuba hayafiki tena chini ya Aswan na wakulima wanahitaji kununua mbolea wa chumvi waliporidhika zamani na matope yaliyobaki mashambani baada ya mafuriko. Vilevile matope hayo yameanza kujaza nafasi ya ziwa na mjao wake umeendelea kupungua polepole.
Pia delta ya Nile katika Mediteranea haikukua tena lakini imeanza kupungua.
Tanbihi
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ziwa la Nasser kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |