Buku Mkia-mrefu
Mabuku mkia-mrefu ni wanyama wa jenasi Beamys katika nusufamilia Cricetomyinae ya familia Nesomyidae ambao wanafanana na panya, lakini panya ni wanafamilia wa Muridae. Urefu wa mwili ni sm 13-19 na mkia una sm 10-16; uzito ni g 55-150. Wana pochi kwa ndani ya mashavu yao ambazo wazitumia kwa kuweka chakula. Rangi yao ni kijivu hadi kahawia juu na nyupe chini. Hula matunda, makokwa, mizizi na wadudu na hupenda machikichi sana.
Buku mkia-mrefu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 2: |
Spishi
hariri- Beamys hindei, Buku Mkia-mrefu Mdogo (Lesser Hamster-rat au Long-tailed Pouched Rat)
- Beamys major, Buku Mkia-mrefu Mkubwa (Greater Hamster-rat au Greater Long-tailed Pouched Rat)