Panya (Rattus)

Panya
Rattus norvegicus 1.jpg
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia
Familia ya juu: Muroidea (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na vipanya)
Nusufamilia: Murinae
Jenasi: Rattus

Kutoka Wikipedia, ensaiklopidia huru

Panya ni wanyama wenye maumbo madogo, jamii ya wanyama wagugumaji (rodents) wenye mkia mrefu ambao ni wa familia ya juu ya Muroidea. "Panya wa kweli" ni wa jenasi Rattus, na wale ambao ni muhimu kwelikweli kwa binadamu na panya wengi, Rattus rattus, pamoja na panya wa kahawia, Rattus norvegicus. Wanyama wengi wa jenasi ya "rodent" na familia zao pia huitwa panya na wanafanana na vitu vingi na panya wa kweli.

Panya wa kweli hutofautishwa na panya pori kwa ukubwa, huku panya wakiwa wakubwa kidogo kuliko panya pori. Familia ya muroid ni kubwa na tata. Na jina panya (kwa kimombo ‘rat’) na panya pori (kwa kimombo ‘mouse’) yakiwa si maalumu sana katika uainishaji wa wanyama.


Spishi na maelezoEdit

Spishi zinazofahamika za panya ni panya mweusi (Rattus rattus) na panya kahawia (Rattus norvegicus). Kundi hili huitwa kama panya wa Dunia ya Kale ama panya wa kweli na limeanzia huko Asia, panya ni wakubwa kuliko panya pori wa Dunia ya Kale, ambao ni ndugu zao na huwa na uzito zaidi ya gramu 500 mwituni.

Neno “panya" hutumika hata kwa mamalia wadogo ambao si panya wa kweli. Mfano ni panya wa Amerika ya Kusini, spishi kadhaa wanaitwa panya kangaroo, na wengine. Panya kama vile 'Bandicoot rat' (Bandicota bengalensis) ni wanyama wagugumaji (rodents) wanaohusiana na panya lakini si panya wa kweli. Katika nchi za mashariki watu wengi wanatumia panya kama panya wa kufugwa. Hawa ni wale wa spishi R. norvegicus, ambao asili yao ni nyika za China na wakasambaa huko Ulaya, mnamo mwa 1775, kwenye Dunia Mpya. Panya wa kahawia mara nyingi hutumika kwa tafiti. Panya wafugwao huwa watiifu na wasikivu kuliko panya wa kale, pia hupata magonjwa mara kwa mara kotokana na kuzaliana na jamii tofauti.

Wengi wa panya huishi kwenye jamii ya watu. Huwa husababisha upungufu na chakula kwenye nchi zinazoendelea.[1] Hata hivyo panya wasumbufu katika kundi hili ni wachache sana huku wengi wao wanaishi visiwani na wamekuwa hatarini kutokana na kuharibika kwa makazi yao.

Panya wanaoishi mwituni huaminika kuwa wanaweza kubeba baadhi ya magonjwa na kuyapeleka kwenye mamalia wengine; kwa mfano huko Ulaya katika mji kadhaa ugonjwa wa ‘Black Death’ inaaminika kuwa imesababishwa na vimelea vya Yersinia pestis na kubebwa na kunguni wa panya wa tropiki waliokuwa wanajishibisha kwa panya wengi wa Ulaya huko. Panya hawa walitumika kama wasafirishaji tu. Mzunguko huu unaendelea kwa nchi nyingi licha ya magonjwa ya binadamu, panya pia wanahusishwa na magonjwa ya mifugo kama vile homa ya maini ya nguruwe.

Kwa kawaida panya huishi kwa muda wa miaka mitatu, lakini wengi huishi kwa mwaka mmoja tu kutokana na kuwindwa na wanyama wengine.


Kama mifugo ya nyumbaniEdit

 
Panya wa kufugwa.

Panya walianza kufugwa nyumbani tangu karne ya 19. Wengi wao ni panya wa kahawia lakini weusi na ‘Giant pouched rats’ nao pia hufugwa. Panya wafugwao huwa na tabia tofauti ukilinganisha na panya wa mwituni kulingana na vizazi vingapi vimewekwa kama mifugo.[2] Pia panya wafugwao, hawaleti hatari tena ya magonjwa kama mifugo mingine, yaani paka na mbwa. Panya wa kufugwa huwa marafiki na wanaweza kuzoeshwa kufanya kazi mbalimbali.


Kama kiungo cha tafitiEdit

 
Panya mwenye kisukari.

Aina moja ya panya wa maabara inajulikana kama panya Zucker. Panya hawa wanazalishwa wakiwa na uwezo wa kupata kifua kikuu na magonjwa mengine ya binadamu.

Mfano 1895, chuo kikuu cha Clark, Worcester, Massachusetts (Marekani) kilianzisha kundi kubwa la panya weupe kwa ajili ya kujifunza madhara ya chakula na mapungufu mengine ya mwili. Kwa miaka mingi panya wametumika kama viungo vya tafiti za magonjwa mbalimbali na kuongeza ufahamu wetu kuhusu viasilia, magonjwa na madhara ya madawa, na mada nyingine ambazo zimechangia mambo makubwa ya afya ya mwili wa binadamu. Uchunguzi wa mwaka 2007 umebaini kuwa panya wana uwezo na akili ambapo hapo awali ulionekana upo kwa binadamu pekee na baadhi ya wanyama wa kale babu wa binadamu.

Panya wa kufugwa ni tofauti sana na wale wa mwituni. Ni wapole na hung’ata kwa nadra sana. Huvumilia uwepo wa watu wengi na huzaliana mapema na kwa wingi sana. Na ubongo, maini, mafigo, tezi ya adrenali na mioyo yao ni midogo sana. (Barnert 2002).


Kama chakulaEdit

Panya kwa nyakati fulani huweza kutumika kwa chakula. Panya huwa chanzo kizuri cha protini kuliko nyama nyingine. Baadhi ya watumwa wa kiafrika huko Amerika ya Kusini walitumia nyama kutosheleza milo yao.[3] Huko Australia watu jamii ya Aborigines, wanatumia panya kwenye milo yao[4] na huko India wanawake wa jamii ya Mishmi, hutumia panya sababu huruhusiwa kula nyama ya samaki, nguruwe na panya tu.[5] Shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa lilikadiria kuwa panya wanafanya zaidi ya nusu ya kiasi cha nyama kinachotumiwa na Waghana. Hakuna marufuku kubwa ya kula panya kwa watu wa magharibi, lakini watu wa jamii ya Shipibo wa Peru na watu wa Sirionó wa Bolivia ndio huwa na marufuku kula panya.[6][7]

Panya pia huliwa na nyoka, na wanyama wengine walao nyama. Jamii mbili za chatu hula panya pekee. Wakati mwingine panya hupatikana sana kwa watu wanaomiliki/wanaofuga wanyama wengine ambapo hutumia panya kama chakula cha wanyama wao.

Kwenye tamaduniEdit

 
Panya wa asili huruhusiwa kutembea huru kwenye Hekalu la Karni Mata

Panya pia wanahusika sana kwenye tamaduni mbalimbali. Watu wa Roma ya kale hawawatofautishi panya na panya pori, badala yake huwaona tu kama panya wakubwa (Mus Maximus) na panya wadogo (Mus Minimus).

Kwenye tamaduni za masharikiEdit

Huko kwenye nchi ya China, panya ni mmoja kati ya wanyama wa walio kwenye kalenda ya Zodiac ya wachina. Watu waliozaliwa kwenye mwaka wa panya huonwa kuwa wana tabia za panya zikiwemo: ukweli, ukarimu, kiu ya kufanya mambo, hasira ya haraka na ufujaji. Watu waliozaliwa katika mwaka wa panya hupatana sana na watu waliozaliwa miaka ya “nyani” na “nyoka aina ya masons (dragon)”, na kupatana kidogo na “farasi”.

Katika tamaduni za India, panya huonekana ni kama sehemu ya Hekalu la Ganesh. Huko kaskazini-magharibi mwa mji wa Deshnoke wa India, panya katika Hekalu la Karni Mata wanawekwa kama wanaume watakatifu. Wahudumu huwalisha panya hao kwa nafaka na maziwa. Mtu kula chakula kilichoguswa na panya hao huonekana kama baraka toka kwa Mungu.

Uainishaji wa RattusEdit

Jenasi ya Rattus ni ya nusufamilia kubwa sana ya Murinae. Kuna jenera kadhaa ambazo pia huonwa kama ni sehemu ya Rattus: Lenothrix, Anonymomys, Sundamys, Kadarsanomys, Diplothrix, Margaretamys, Lenomys, Komodomys, Palawanomys, Bunomys, Nesoromys, Stenomys, Taeromys, Paruromys, Abditomys, Tryphomys, Limnomys, Tarsomys, Bullimus, Apomys, Millardia, Srilankamys, Niviventer, Maxomys, Leopoldamys, Berylmys, Mastomys, Myomys, Praomys, Hylomyscus, Heimyscus, Stochomys, Dephomys, na Aethomys.

Spishi wa panyaEdit

Sunburned Rat (Rattus adustus) – Kisiwa cha Enggano, Indonesia
Sikkim Rat (Rattus naamanensis) – Butani, Kamboja, Uchina, Uhindi, Laos, Myama, Nepal, Uthai, na Vietnam
Rice-field Rat (Rattus argentiventer) – Asia ya Kusini-Mashariki
Summit Rat (Rattus baluensis) – Malaysia
Bonthain Rat (Rattus bontanus; obs. Rattus foramineus) – Indonesia
Nonsense Rat (Rattus burrus) – Uhindi
Dusky Rat (Rattus colletti) – Australia
Sula Rat (Rattus elaphinus) – Indonesia
Enggano Rat (Rattus enganus) – Indonesia
Philippine Forest Rat (Rattus everetti) – Ufilipino
Polynesian Rat (Rattus exulans) – Fiji na Visiwa vingi vya Polynesia, Nyuzilandi, Kisiwa cha Pasaka, Visiwa vya Hawaii
Spiny Ceram Rat (Rattus feliceus) – Indonesia
Bush Rat (Rattus fuscipes) – Australia
Giluwe Rat (Rattus giluwensis) – Papua Guinea Mpya
HaiFamiliald's Rat (Rattus haiFamilialdi) – Indonesia
Hoffmann's Rat (Rattus hoffmanni) – Indonesia
Hoogerwerf's Rat (Rattus hoogerwerfi) – Indonesia
Japen Rat (Rattus jobiensis) – Indonesia
Koopman's Rat (Rattus koopmani) – Indonesia
Korinch's Rat (Rattus korinchi) – Indonesia
Cape York Rat (Rattus leucopus) – Australia, Indonesia, na Papua Guinea Mpya
Lesser Rice-field Rat (Rattus losea) – Uchina, Laos, Taiwan, Uthai, na Vietnam
Mentawai Rat (Rattus lugens) – Indonesia
Australian Swamp Rat (Rattus lutreolus) – Australia
Maclear's Rat (Rattus macleari) – Kisiwa cha Krismasi
Opossum Rat (Rattus marmosurus) – Indonesia
Mindoro Black Rat (Rattus mindorensis) – Ufilipino
Little Soft-Furred Rat (Rattus mollicomulus) – Indonesia
Nillu Rat (Rattus montanus) – Sri Lanka
Eastern Rat (Rattus mordax) – Papua Guinea Mpya
Molaccan Prehensile-tailed Rat (Rattus morotaiensis) – Indonesia
Bulldog Rat (Rattus Familiativitatis) – Kisiwa cha Krismasi
Moss-forest Rat (Rattus niobe) – Papua Guinea Mpya, Indonesia
Himalayan Field Rat (Rattus nitidus) – Bangladesh, Butani, Uchina, Uhindi, Indonesia, Laos, Myama, Nepal, Palau, Ufilipino, Uthai, na Vietnam
Brown Rat or Norway Rat (Rattus norvegicus) – duniani kote ghairi ya Antarctica
New Guinean Rat (Rattus novaeguineae) – Papua Guinea Mpya
Osgood's Rat (Rattus osgoodi) – Vietnam
Palm Rat (Rattus palmarum) – Uhindi
Peleng Rat (Rattus pelurus) – Indonesia
Spiny Rat (Rattus praetor) – Indonesia, Papua Guinea Mpya, na Visiwa vya Solomon
Turkestan Rat (Rattus pyctoris; obs. Rattus turkestanicus) – Afghanistan, Uchina, Uhindi, Iran, Kyrgyzstan, Nepal, na Pakistan
Kerala Rat (Rattus ranjiniae) – Uhindi
Black Rat (Rattus rattus) – duniani kote ghairi ya Antarctica
Glacier Rat (Rattus richardsoni) – Indonesia
Sikkim Rat (Rattus sikkimensis) – Butani, Kamboja, Uchina, Uhindi, Laos, Myama, Nepal, Uthai, na Vietnam
Simalur Rat (Rattus simalurensis) – Indonesia
Dusky Field Rat (Rattus sordidus) – Australia, Indonesia, na Papua Guinea Mpya
Stein's Rat (Rattus steini) – Indonesia na Papua Guinea Mpya
Naaman Rat (Rattus stoicus) – Visiwa vya Naaman
Tanezumi Rat (Rattus tanezumi) – Afghanistan, Bangladesh, Kamboja, Uchina, Kisiwa cha Cocos (Keeling), Fiji, Uhindi, Indonesia, Japani, Korea ya Kaskazini, Korea ya Kusini, Laos, Malaysia, Myama, Nepal, Pakistan, Ufilipino, Taiwan, Uthai, na Vietnam
Tawi-Tawi Forest Rat (Rattus tawitawiensis) – Ufilipino
Timor rat (Rattus timorensis) – Timor
Malayan Field Rat (Rattus tiomanicus) – Indonesia, Malaysia, Ufilipino, na Uthai
Pale Field Rat (Rattus tunneyi) – Australia
Van Deusen's Rat (Rattus vnaeuseni) – Papua Guinea Mpya
Slender Rat (Rattus verecundus) – Indonesia na Papua Guinea Mpya
Long-Haired Rat (Rattus villosissimus) – Australia
Yellow-Tailed Rat (Rattus xanthurus) – Indonesia

MarejeoEdit

  1. Meerburg BG, Singleton GR, Leirs H (2009). "The Year of the Rat ends: time to fight hunger!". Pest Manag Sci 65 (4): 351–2. doi:10.1002/ps.1718 . PMID 19206089 . http://www3.interscience.wiley.com/journal/121686000/abstract.
  2. Wild Rats in Captivity and Domestic Rats in the Wild. Ratbehaviour.org. Iliwekwa mnamo 2009-07-04.
  3. Otto, John Solomon; Augustus Marion Burns III. (December 1983) Black Folks, and Poor Buckras: Archeological Evidence of Slave and Overseer Living Conditions on an Antebellum Plantation. Journal of Black Studies, Vol. 14, No. 2. pp. 185-200
  4. Hobson, Keith A.; Stephen Collier. (April 1984) Marine and Terrestrial Protein in Australian Aboriginal Diets. Current Anthropology, Vol. 25, No. 2. pp. 238-240
  5. Mills, J. P. (January 1952) The Mishmis of the Lohit Valley, Assam. The Journal of the Royal Anthropological Institute of Great Britain and Ireland, Vol. 82, No. 1. pp. 1-12
  6. Behrens, Clifford A. (September 1986) Shipibo Food Categorization and Preference: Relationships between Indigenous and Western Dietary Concepts. American Anthropologist, Nathan New Series, Vol. 88, No. 3. pp. 647-658.
  7. Priest, Perry N. (October 1966) Provision for the Aged among the Sirionó Indians of Bolivia. American Anthropologist, New Series, Vol. 68, No. 5. pp. 1245-1247