Bulawayo ni mji mkubwa wa pili wa Zimbabwe wenye wakazi 665,940 (sensa ya 2022[1]). Iko kusini-magharibi ya nchi hiyo, katikati ya Matabeleland. Wakazi walio wengi ni Wandebele.

Bendera ya Bulawayo
Mahali pa Bulawayo
"Picha hii ilipigwa wakati wa ziara ya Bulawayo, Rhodesia, sasa Zimbabwe, na watu wawili ambao baadaye walitibiwa ugonjwa wa Marburg. Picha hii ilipigwa Februari 2 au 3, 1975, usiku wa pili au wa tatu baada ya mgonjwa wa virusi vya Marburg #1 kufika. kuwasiliana na vekta isiyojulikana."

Jina la mji linatokana na neno la Kindebele "Kwabulawayo" yaani "machinjoni".

Historia hariri

Mji wa leo ulijengwa juu ya mabaki ya boma la mfalme Lobengula. Lobengula aliwahi kujenga boma lake la kwanza 1871 takriban kilomita 15 kusini ya mji. Mwaka 1881 alihamia penye mji wa sasa.

Mwaka 1893 ufalme wa Lobengula ulishambuliwa na jeshi la Cecil Rhodes na mfalme aliamua kuchoma boma lake alipoona alishindwa kuzuia maadui. Waingereza walianzisha mji wao juu ya mabaki ya makazi ya awali. 1897 ilipewa cheo cha manisipaa na kuungwa na reli.

Bulawayo ilikuwa mji ambako upinzani dhidi ya ukoloni ulianza na baadaye kitovu cha upinzani dhidi ya serikali ya Robert Mugabe.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bulawayo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.