Wandebele
Wandebele ni jina la makundi mawili ya wasemaji wa lugha za Kibantu zinazofanana na Kizulu.
- Wandebele wa Afrika Kusini huishi Afrika Kusini katika majimbo ya Mpumalanga, Gauteng na Limpopo. Hujiita wenyewe amaNdebele, lugha yao huitwa "Kindebele cha Kusini".
- Wandebele wa Zimbabwe walihamia pale wakati wa Mfecane yaani kipindi cha mvurugo kilichosababishwa na vita vya Shaka Zulu. Lugha yao hutiwa "Kindebele cha Kaskazini" na leo hii ni lugha kubwa ya pili ya Zimbabwe baada ya Kishona.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wandebele kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |