Seresi (sayari kibete)

asteroidi
(Elekezwa kutoka Ceres (sayari kibete))

Seresi (alama: ⚳[1]) ni sayari kibete ndogo inayojulikana katika mfumo wa jua letu na sayari kibete ya pekee iliyoko ndani ya ukanda wa asteroidi. Jina rasmi katika orodha ya sayari ndogo ni 1 Seresi.[2]

1 Seresi ilivyopigwa picha na kipimaanga "Dawn"
Nafasi ya Seresi kati ya sayari kwenye mfumo wa jua

Uvumbuzi na jina

hariri

Ilivumbuliwa 1 Januari 1801 na Giuseppe Piazzi[3] aliyeiona kama sayari kamili. Piazzi aliteua jina lake kutokana na mungu wa Kiroma wa kike Ceres aliyehusika na mambo ya ustawi wa mimea hasa ya kilimo, mavuno na upendo wa kimama. Katika mwendo wa karne ya 19 magimba mengi mengine yalivumbuliwa hasa katika ukanda kati ya Mrihi na Mshtarii kwa hiyo wanaastronomia walipatana kutumia majina kama asteroidi au pia planetoidi kwa ajili ya magimba yale madogo. Kwa ajili asteroidi hizi ilikuwa kawaida kuweka namba mbele ya jina lenyewe na Seresi iliyokuwa asteroidi ya kwanza iliyovumbuliwa ilipata namba "1" hivyo jina lake likawa "1 Seresi".

Miaka 200 baada ya uvumbuzi wake 1 Seresi ilipangwa katika jamii ya sayari kibete lakini hadi wakati ule ilitazamiwa kama asteroidi kubwa.

Ina kipenyo cha kilomita 950 hivyo ni gimba kubwa kabisa ndani ya ukanda wa asteroidi. Sababu ya kuihamisha katika kundi la sayari kibete ni inaonyesha umbo la tufe kama sayari. Uzito wa mada yake unasababisha kiwango cha graviti cha kutosha ili kusawazisha umbo lake kuwa karibu na tufe, tofauti na magimba madogo yanayoonekana kwa maumbo mbalimbali bila muundo maalumu.

Haing'ai sana maana pamoja ya umbali wake uso wake unakosa tabia ya kuakisi nuru ya kotosha ili kuonekana bila msaada wa darubini. [4]

Tarehe 27 Septemba 2007 NASA ilirusha chombo cha angani Dawn Mission kwa shabaha ya kukaribia 1 Seresi pamoja na asteroidi kubwa ya 4 Vesta.

Marejeo

hariri
  1. JPL/NASA (2015-04-22). "What is a Dwarf Planet?". Jet Propulsion Laboratory. Iliwekwa mnamo 2022-01-19.
  2. Sayari kibete pamoja na vyote vinavyotazamiwa kuwa "visayari" vinapewa namba kabla ya jina lenyewe.
  3. Piazzi, Giuseppe (1801). Risultati delle osservazioni della nuova Stella scoperta il dì 1 gennajo all'Osservatorio Reale di Palermo (kwa Italian). Palermo.{{cite book}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  4. Ceres at Solarviews.com