NASA ni kifupi cha Kiingereza cha "National Aeronautics and Space Administration" (Mamlaka ya Taifa ya Uanahewa na Ange-nje). Mamlaka hii ilianzishwa 1958. Wajibu wake ni kusimamia miradi ya serikali ya Marekani ya kuendesha utafiti na uchunguzi wa anga. NASA inasimamia utengenezaji wa roketi za kurusha vyombo vya angani na utengenezaji wa vyombo vya angani vyenyewe.

Roketi iliyorusha "Freedom 7" na Alan Shepard Jr.angani tar. 5.5.1961

Miradi ya NASA ilianzishwa kutokana na Mshtuko wa Sputnik yaani baada ya Warusi kushtusha dunia kwa kupeleka vyombo vya angani vya kwanza katika mradi wao wa Sputnik. Uliofuatiwa na mradi wa "Vostok" ambao tarehe 12 Aprili 1961 ulimfikisha Yuri Gagarin angani akiwa mtu wa kwanza kwenda angani.

Mradi wa kwanza wa NASA ulikuwa Mradi wa Mercury uliotakiwa kuonyesha ya kwamba wanaanga wanaweza kukaa angani kwa muda fulani. Alan B. Shepard Jr. alikuwa Mmarekani wa kwanza angani kwa muda wa dakika 15; John Glenn alikuwa Mmarekani wa kwanza wa kuzunguka dunia tarehe 20 Februari 1962 kwa chombo cha angani "Friendship 7".

Mradi huo ulifuatiwa na Mradi wa Gemini kuanzia mwaka 1965 ulionyesha ya kwamba watu wanaweza kukaa angani kwa muda wa siku kadhaa hata kutekeleza shughuli fulani. Gemini iliandaa Mradi wa Apollo uliopeleka watu wa kwanza mwezini. Chombo cha angani "Apollo 11" kilifikisha wanaanga Neil Armstrong na Buzz Aldrin kwenye uso wa mwezi tarehe 20 Julai 1969 na kuwarudisha dunia tena.

Tangu mwanzo ule kuna miradi mingi iliyofuata.

Buzz Aldrin akitembea kwenye uso wa mwezi wakati wa safari ya Apollo 11.

Viungo vya nje