Chekecha Cheketua
"Chekecha Cheketua" ni jina la wimbo uliotoka 29 Juni 2015 wa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Ali Kiba. Wimbo umetayarishwa na Abby Daddy ukiwa wimbo wa pili kutolewa tangu kusimama kutoa kazi za kujitegemea miaka mitatu iliyopita. Video ya wimbo huu imeongozwa na Meji Alabi ambaye Kiba anamsifia kwa kusema anamuelewa sana kupita maelezo. Huu ulikuwa wimbo wa kwanza kufanya kazi na Meji ukafuatiwa na Aje kisha Aje Remix. Vilevile ni video ya pili kufanyiwa nchini Afrika Kusini. Hadi wimbo huu kutoka, Kiba bado ameweza kushikilia misingi ya Bongo Flava bila kutia vionjo vya nyimbo au uigizaji wa nyimbo za Afrika Magharibi. Wakati sehemu kubwa ya wasanii wa Tanzania wamekuwa wakiangukia mikononi mwa muundo wa muziki wa Nigeria na Ghana.[1]
“Chekecha Cheketua” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kava ya Chekecha Cheketua
| |||||
Single ya Ali Kiba | |||||
Imetolewa | 29 Juni, 2015 | ||||
Muundo | Upakuzi wa mtandaoni | ||||
Imerekodiwa | 2015 | ||||
Aina | Pop, Bongo Flava | ||||
Urefu | 3:30 | ||||
Studio | RockStar4000 | ||||
Mtunzi | Ali Kiba | ||||
Mtayarishaji | Abby Daddy | ||||
Mwenendo wa single za Ali Kiba | |||||
|
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Wakati wasanii wengi kwa sasa wakiiga vibwagizo vya Nigeria JamiiForum mnamo 27 Februari, 2015. Miezi minne kabla ya wimbo kutoka.
Viungo vya nje
hariri- Chekecha Cheketua katika YouTube