Chembeuzi Y (pia: kromosomu Y, kwa Kiingereza Y chromosome) ni moja katika jozi la chembeuzi za jinsia za wanyama wengi kujumuisha mamalia, na kwa hivyo binadamu pia, pamoja na chembeuzi X. Ndizo zinazosababisha mtu kuwa mwanamume au mwanamke, na vilevile wanyama mbalimbali kuwa wa kiume au wa kike.

Human Y chromatid.

Baba tu ana chembeuzi hiyo (pamoja na ile ya X) na hivyo anaweza kumrithisha mwanae, ambaye kwa njia hiyo atakuwa wa kiume. Kumbe mama ana jozi la chembeuzi X asiweze kurithisha chembeuzi Y.

Utafiti unaonyesha kwamba chembeuzi Y ni kati ya sehemu za urithi wa binadamu zinazobadilika zaidi.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chembeuzi Y kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.