Cheusi Mtungi
Cheusi Mtungi ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Godliver Gordian. Cheusi ni mke halali wa Cheche Mtungi. Anapitia magumu mengi kwenye ndoa yake lakini anayatatua kwa aina yake. Sifa kuu ya Cheusi ni uvumilivu wake katika ndoa - hasa ukizingatia mumewe ni mtu wa wanawake sana. Sifa nyengine aliyonayo ni pamoja na upole na unyenyekevu kwa mume na mama yake mzazi Bi. Mwanaidi. Hapendi kuyumbishwa kwa ndoa yake na mtu yeyote yule hata kama ni mama yake mzazi ndiye myumbishaji.[1] Kwa upande wa familia aliyozaliwa, yeye ni mtoto wa kwanza wa Bi. Mwanaidi ambaye ni mke wa pili wa Mzee Kizito. Cheusi ni dada wa Shoti, ambaye anaonekana kidogo kuwa na kautahira.
Cheusi Mtungi | |
---|---|
muhusika wa Siri ya Mtungi | |
Taswira ya Cheusi Mtungi (uhusika umechezwa na Godliver Gordian | |
Imebuniwa na | MFDI Tanzania |
Imechezwa na | Godliver Gordian |
Misimu | 1, 2 |
Maelezo | |
Jinsia | Kike |
Kazi yake | Mama wa nyumbani |
Ndoa | Cheche Mtungi |
Watoto | 3 |
Ndugu | Shoti |
Dini | Mwislamu |
Utaifa | Mtanzania |
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Cheusi Mtungi Archived 12 Septemba 2016 at the Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.