Mzee Kizito ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Nkwabi Ng'hangasamala. Mzee Kizito ni mtu mwema, mwenye moyo wa huruma kwa kila mja aliyekaribu nae. Ana nyumba tatu. Moja Bi. Farida, Bi. Mwanaidi na Nusura. Vilevile anamiliki gereji ambayo anafanya kazi na watoto zake. Ni moja kati ya wazee wanaofuata maadili mno, tena hapendi kuyumbishwa wala kuyumbisha. Msema kweli kwa kila linalomfika.

Mzee Kizito
muhusika wa Siri ya Mtungi

Taswira ya Mzee Kizito (uhusika umechezwa na Nkwabi Ng'hangasamala)
Imebuniwa na MFDI Tanzania
Imechezwa na Nkwabi Ng'hangasamala
Idadi ya sehemu 26
Misimu
1, 2
Maelezo
Jinsia Kiume
Kazi yake Fundi makenika gereji
Ndoa Bi. Farida
Bi. Mwanaidi
Vingawaje
Nusura
Watoto Cheusi Mtungi
Shoti
Sabrina Kizito (jumla wapo 17)
Dini Mwislamu
Utaifa Mtanzania

Hasa hupenda kumwambia mambo mengi sana mke wake wa pili Bi. Mwanaidi. Alijikuta anaingia matatani na wimbo zito la mawazo baada ya kumuoa Nusura na kupata taarifa ya kuwa ana UKIMWI. Haitoshi, Bi. Farida nae katika hangai yake ya kutaka kumroga mumewe, kalivagaa gono kutoka kwa mganga wa kienyeji na kulileta nyumbani na hatimaye Kizito kulipata haraka pindi tu alipojamiiana na mke wake wa kwanza.

Ana mahusiano ya wastani na mkwewe Cheche Mtungi. Ndiye aliyemwezesha kufungua upya Studio ya Mtungi. Rafiki wake wa karibu ni Mjomba (Seif Mbembe), ambaye ndiye hasa anayemtegemea katika kutekeleza mambo yake mengi sana. Mjomba ndiye aliyefanikisha zoezi la kumtolea posa Nusura hapo awali. Hata alivyopata gono, haraka alimwendea Mjomba na kumweleza yanayomsibu na bila kusita Mjomba alimshauri aende hospitali kujitazama. Kwa ujumla wake, Kizito hana shida na mtu. Ana urafiki na kila lika. Mara kadhaa Duma ameonekana kwenda kuazima gari la Mzee Kizito na kulifanya vibaya na bado aliendelea kumpa.[1]

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Mzee Kizito Ilihifadhiwa 12 Septemba 2016 kwenye Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.