Cheche Mtungi
Cheche Mtungi ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Juma Rajab Rashid. Cheche ni muhusika mkuu katika tamthilia hii. Anaongoza kwa mikasa ya kila aina. Ijapokuwa ameonekana kuishinda kila wakati. Cheche ni mpiga picha mahiri ana asiyependa kuharibu kazi yake.
Cheche Mtungi | |
---|---|
muhusika wa Siri ya Mtungi | |
Taswira ya Cheche Mtungi (uhusika umechezwa na Juma Rajab Rashid | |
Imebuniwa na | MFDI Tanzania |
Imechezwa na | Juma Rajab Rashid |
Misimu | 1, 2 |
Maelezo | |
Jinsia | Kiume |
Kazi yake | Mpiga picha |
Ndoa | Cheusi Mtungi |
Watoto | 3 |
Dini | Mwislamu |
Utaifa | Mtanzania |
Muhtasari wa uhusika
haririKazi ya upigaji picha alifundishwa na marehemu mzee Habibu aliyekuwa anamtumia Cheche kama msadizi wake, halafu baadaye kama mtu aliyemrithisha studio kienyeji. Ukweli halisi kuwa studio ni mali ya Cheche ilikuja kujulikana kwenye sehemu ya 26 ambapo Cheche alipata usia wa Mzee Habibu kauficha darini katika mazingira ya utata. Usia unataja mali zote ni za Shalima isipokuwa studio ni urithi halali wa Cheche. Mzee Habibu aliiacha studio mikononi mwa Cheche. Lakini awali alishindwa kuiendeleza hadi hapo alipoamua kuirudia na kuipa jina la Mtungi Studio na kuondoa jina la "Habib Studio". Ujuzi aliouchukua kwa Mzee Habibu ni mkubwa sana. Cheche si mbabaishaji katika suala zima la upigaji picha.
Anapenda kuona wateja wake wanafurahia huduma yake ya upigaji picha. Halkadhalika Cheche hapendi matatizo. Hata ukimdhulumu yeye huwa kimya anakuacha na balaa lako. Mfano mmoja waliomdhulumu ni Bonge aliyesimama kama meneja wa Sharo Milionea na wa pili Mama Azimara aliyemwalika katika ngoma ya mwanae, bahati mbaya Cheche akatoweka shughulini na kwenda kichakanani kufanya zinaa na Greta msichana aliyekutana nae ngomani hapo. Pamoja na kutoweka, lakini bado alitengeneza DVD ya ngoma hiyo na malipo hakuna kaambulia vitisho na ubabe wa mtoto wa mjini Mama Azimara.
Cheche ni mtu wa wanawake sana, lakini pia anampenda sana mkewe na watoto zake. Cheche ni baba wa watoto watatu watundu balaa. Katika suala zima la kupenda wanawake, Cheche ameonekana kushindwa kabisa kujizuia anapoona totozi. Mkewe anafahamu kama Cheche mtu wa wanawake, lakini ana mvumilia kwa sababu wanapendana kwa dhati licha ya madhila ya kutoka nje ya ndoa. Jambo hili la Cheche kupenda wanawake, lilipelekea mkewe Cheusi Mtungi kujiunga na programu ya uzazi wa mpango na kuwekewa kitanzi cha kuzuia mimba hadi hapo atakapokuwa tayari.
Cheche anapenda sana watu. Mpole na mcheshi. Mwenye majibu ya utata mara kwa mara. Ana mahusiano na Tula, Lulu na Greta aliyekutana nae ngomani. Mara nyingi shida zake ndogondogo huwa anampelekea Tula aliyeonekana kumshauri mambo mengi ya maisha na kifamilia pia. Tula anampenda sana Cheche, shida hana uhuru nae. Isitoshe, Tula anajitoa mazima kwa Cheche. Cheche hataki mahaba niue katika hili kisa tu anamhofia mkewe. Tula anaonekana kunogewa sana na mapenzi ya Cheche, anatumia nguvu nyingi kumdhibiti Cheche, hili linamfanya Cheche apunguze safari za kwenda kwa Tula.
Mahusiano yake na Lulu ni ya kuzima na kuwasha. Lulu akijisikia, anamtafuta Cheche, kwa uzuri wa Lulu, Cheche daima alishindwa kukataa wito. Lakini Lulu ni gumzo katika mji mzima. Nani asiyejua kuwa Lulu ni kicheche, lakini bila kujali Cheche hajivungi kwake. Mahusiano ya Cheche na Lulu yalifika hadi nyumbani kwa mama watoto wake Bi. Cheusi. Mama wa Cheusi, Bi. Mwanaidi, alizikuta picha za Lulu zilizopigwa na Cheche chumbani kwa Shoti na kuzichukua na kumpelekea binti yake aone jinsi mume wake alivyo si mwaminifu.
Awali Cheusi alikubali, lakini baadaye alizikataa kwa kuwa aliona haina maana hata akijua ukweli wa mumewe ni malaya. Anampenda mumewe na matatizo yao watayamaliza wenyewe kama wanandoa. Cheche ni mtu mwenye kupendwa na kila mwanamke aliyekaribu nae. Tena kila anayejitokeza hajui kuvunga. Ana urafiki wa karibu na rafiki yake kipenzi Dafu ambaye ni fundi umeme na mtu mwenye kutaka kujua mambo mengi ya Cheche na ya mtaani.
Cheche ni mume wa Cheusi, shemeji yake na Shoti aliyezaliwa na Cheusi kwa Bi. Mwanaidi. Mkwe wake Mzee Kizito mwenye wake watatu, Bi. Farida, Bi. Mwanaidi na Nusura. Hana marafiki wengi zaidi ya Dafu ambaye mara kwa mara anamtegemea katika masuala yake binafsi na mambo mengine mbalimbali.[1]
Kazi
haririStudio
haririCheche ni mpiga picha mahiri kabisa. Ana sifa ya kipekee kwa upigaji picha wake. Tena haridhiki na kupiga picha moja tu bali mbalimbali walau aipate ile ambayo anaona kwako itakuwa bora zaidi. Awali studio ilionekana kama vile karithi katika mazingira ya utata. Sehemu za mwanzo hazikuonesha kabisa umiliki halali wa Cheche katika studio hiyo. Ndiyo maana hata Shalima alivyokuja kuonekana katika sehemu ya 12 kama utambulisho na sehemu ya 13 kaja kudai kuwa studio ni mali yake. Urithi kutoka kwa marehemu babake Mzee Habibu. Lakini utata huu ulikuja kumalizika baada ya Cheche kukuta nyaraka rasmi za mzee Habibu kaandika usia mwenyewe kuwa Cheche Mtungi ndiye mmiliki wa studio na si mtu mwingine yeyote yule. Hii ilikuja kuonekana kwenye sehemu ya 26 ya msimu wa pili.
Aina ya wateja (bila Shalimar)
haririKabla ya ujio wa Shalimar, Cheche alikuwa anapiga picha kwa watu wa aina mbalimbali bila kubagua. Kipindi hiki kilikuwa kigumu sana kwa Cheche, magumu ya maisha aliyaona kwa kasi ya ajabu. Huku familia, mara tatizo hili mara lile. Bado tabia zake nazo wa kupenda wanawake ilikuwa changamoto kubwa mno. Kazi hii ya studio ndio hasa maisha ya Cheche.
Akiwa na Shalimar
haririTangu ujio wa Shalimar, mambo yamekuwa yanaenda kitaalamu zaidi. Sehemu kubwa ya wateja wakawa warembo kwa ajili ya mtangazo ya taasisi mbalimbali za ulimbwende. Wakati huu ulikuwa mgumu sana kwa Cheche. Hasa ukizingatia kumekuwa na migogoro mingi na mama watoto wake dhidi ya tabia za kupenda wanawake. Kazi inakuwa ngumu kwa Cheche kwa vile picha nyingi zinazopigwa na warembo hawa huwa aidha za kukaa uchi au nusu uchi. Majaribu yamekuwa mengi, lakini hatimaye anaweza kuyashinda. Kibaya zaidi, Lulu ndiye amekuwa Meneja wa Studio. Suala hili lilileta mtafaruku mkubwa kati yake na Cheusi. Ilifikia hatua hakuna hata kupeana unyumba kwa kuhofia maambukizi ndani ya nyumba. Tangu Shalimar abadili muundo wa studio, Cheche amekuwa mtoro hakuna mfanowe. Cheche hakupendezewa na usimamizi wa Shalimar, japo Shalimar anajitia hana wasiwasi na Cheche. Baadaye wakaanza kuelewana huku siku si nyingi akapata wasia halisi aliouacha marehemu Mzee Habibu kuhusu urithi wa studio. Hadi msimu wa pili unaisha, Cheche kapiga picha warembo wengi hakuna mfano.
Mahusiano na familia
haririCheche ana mahusiano mazuri sana na mkewe. Licha ya kuwa na mashindano ya hapa na pale. Cheche anaipenda sana familia yake, lakini pia anapenda wanawake wengi. Cheche ana watoto watatu, Maua, Mkuki na Tea. Anaipenda sana familia yake. Ana mapenzi mazito na mkewe. Japo mara kwa mara hulumbana kwa mambo tofauti hasa kuhusu umalaya wa Cheche na nongwa za mama mkwe wake.
Mahusiano yake na Tula
haririTula ni msichana wa Cheche wa kwanza. Kwa mara ya kwanza Cheche alianza mapenzi na Tula kabla ya kuja kumuoa Cheusi. Tula ni mjasiriamali anayejishughulisha na kijigrosari, mshauri mzuri wa Cheche na mvumilivu wa kila hali. Tula anampenda sana Cheche, ila tu, Cheche anamgeuza Tula kama spea tairi. Akiwa na hamu zake, mbio kwa Tula. Hali hii ilimfanya Tula aone hakuna mustakabali mzuri na Cheche. Isitoshe, Cheche ni mume wa mtu, yeye nae ana muhitaji kila wakati awe nae, lakini inashindikana. Bado anasikia kashfa za Cheche kuwa na wanawake wengi.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Cheche Mtungi Ilihifadhiwa 12 Septemba 2016 kwenye Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.