Chitungwiza

Chitungwiza ni mji mchanga katika Zimbabwe. Iko kilometa 9 upande wa kusini wa mji mkuu Harare. Mwaka 2006 ilikuwa na wakazi 425,000. Walio wengi wanafanya kazi Harare kwa sababu kuna nafasi chache tu za ajira.

Kituo cha manunuzi Chitungwiza

Chitungwiza ilipata cheo cha manispaa mwaka 1981. Asili yake ni mitaa mitatu ya Seke, Zengeza na St Marys iliyojengwa wakati wa ubaguzi wa rangi kama makazi ya Waafrika wasioruhusiwa kukaa Harare penyewe.

Siku hizi Chitungizwa ni mji wa kukua haraka Zimbabwe. Kiwanja cha ndege cha Harare kipo karibu. Wapiga kura wa mji walisimama kwa upande wa upinzani wa MDC (Movement for Democratic Change) wakati wa chaguzi tangu mwaka 2000.

External linksEdit