Manispaa (kwa Kiingereza: municipality) ni mji wenye kiwango fulani cha kujitawala katika shughuli zake.

Manispaa za jiji la dar es salam
Ramani ya manispaa za Italia
Manispaa

Madaraka hayo ni pamoja na haki ya kutawaliwa na serikali ya mahali iliyochaguliwa na watu wa manispaa (badala ya kusimamiwa na mwakilishi wa serikali kuu) kuamulia na kukusanya kodi fulani katika eneo la maniipaa na kupanga makisio yake yenyewe.

Manispaa za Tanzania

hariri

Nchini Tanzania manispaa ni mji wenye wakazi zaidi ya 100,000 hadi 500,000.

Katika muundo wa utawala manispaa za Tanzania zinahesabiwa kama wilaya. Serikali ya manispaa huitwa Halmashauri ya manispaa (Municipal Council).

Manispaa za Tanzania ni Bukoba, Dodoma, Iringa, Kahama, Kigoma, Lindi, Morogoro, Moshi, Mtwara, Musoma, Shinyanga, Singida, Songea, Sumbawanga na Tabora.

Halafu kuna manispaa saba ambazo ni sehemu ya majiji mawili.

  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Manispaa kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.