Chuo Kikuu cha Jos

Chuo Kikuu cha Jos, kinachojulikana kwa kifupi kama Unijos, ni chuo kikuu cha shirikisho kilichopo Jos, Jimbo la Plateau, katikati ya Nigeria.

Historia

hariri

Kilichokuwa Chuo Kikuu cha Jos kilianzishwa mnamo Novemba 1971 kutoka kwenye kampasi ya satellite ya Chuo Kikuu cha Ibadan. Wanafunzi wa kwanza walipokelewa mnamo Januari 1972 kama wanafunzi wa kabla ya shahada na programu ya kwanza ya Shahada ya Sanaa ilianza mnamo Oktoba 1973. Mnamo Oktoba 1975, serikali ya kijeshi ya wakati huo chini ya Jenerali Murtala Mohammed ilianzisha Unijos kama taasisi tofauti. Makamu Mkuu wa kwanza wa Unijos alikuwa Profesa Gilbert Onuaguluchi. Masomo yalianza katika Chuo Kikuu cha Jos kilichopangwa upya mnamo Oktoba 1976 na wanafunzi 575 waliotapakaa kwenye vitivo vinne vilivyokuwepo vya Sanaa na Sayansi ya Jamii, Elimu, Sayansi Asilia na Sayansi ya Tiba. Programu za baada ya shahada ziliongezwa mnamo 1977. Kufikia mwaka 1978, Vitivo vya Sheria na Sayansi ya Mazingira vilianzishwa na Vitivo vya Sanaa na Sayansi ya Jamii vilitenganishwa.

Mnamo 2003, Shirika la Carnegie la New York liliipa Unijos ruzuku ya dola milioni 2 ili kuanzisha idara yake ya kukusanya fedha.

  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Jos kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.