Chuo Kikuu cha Ufundi cha Berlin
(Elekezwa kutoka Chuo Kikuu cha Ufundi Berlin)
Chuo Kikuu cha Ufundi Berlin (jer. Technische Universität Berlin, kifupi TU Berlin, ing. Technical University of Berlin) ni kimoja cha vyuo vikuu mjini Berlin, Ujerumani.
Mwaka 2018 chuo hiki kilikuwa na wanafunzi 33,577 na theluthi moja walikuwa wanawake[1]. Takriban robo moja walikuwa wanafunzi wasio Wajerumani hasa kutoka China, Urusi, Uturuki na nchi za Afrika.
Chuo kilianzishwa mwaka 1879 kama chuo cha Prussia, wakati ule dola kubwa la Ujerumani. Wanafunzi na walimu kumi wa chuo hiki waliendelea kupokea Tuzo ya Nobel katika fani za fizikia na kemia ambao ni Adolf von Baeyer, Carl Bosch, Dennis Gabor, Ernst Ruska, Eugene Paul Wigner, Fritz Haber, George de Hevesy, Gerhard Ertl, Gustav Hertz, Wolfgang Paul[2].
Tanbihi
hariri- ↑ Student Enrollment Statistics (June 2018, tovuti ya TUB, iliangaliwa 1 Desemba 2018
- ↑ University History, kwenye tovuti ya TUB, iliangaliwa 1 Desemba 2018
Viungo vya Nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Ufundi cha Berlin kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |