Collision (Heroes)
"Collision" ni sehemu ya nne ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa ubunifu wa kisayansi unaorushwa hewani na kituo cha televisheni cha NBC, Heroes. Kipengele hiki awali kilipewa jina la "Come Together".
"Collision" | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Sehemu ya Heroes | |||||||
Mjumbe anayetoka baadaye kaleta ujumbe kwa kwa Peter. | |||||||
Sehemu ya. | Msimu 1 Sehemu 4 | ||||||
Imetungwa na | Bryan Fuller | ||||||
Imeongozwa na | Ernest Dickerson | ||||||
Tayarisho la | 104 | ||||||
Tarehe halisi ya kurushwa | 16 Oktoba 2006 | ||||||
Waigizaji wageni | |||||||
| |||||||
Orodha ya sehemu za Heroes |
Hadithi (kwa ufupi)
haririMatt Parkman ni mfungwa wa Mr. Bennet na mtu asiyejulikana. Pale ilipogundulika kwamba Matt anajua yale ya Claire, yule mtu asiyejulikana kapewa kazi ya "Kufuta kumbukumbu za Matt", kwa mchakato wenyewe maumivu makali.
Hiro na Ando wanawasili mjini Las Vegas. Watakuwa wanakaa kwenye Montecito Hotel na Casino. Ando anamsaidia Hiro na jumbe za onyo kwa Isaac Mendez, hivyo basi Isaac atajua kwamba yeye na jiji la New York wapo hatarini.
Wamempitia Niki Sanders na mtoto wake Micah, ambao wapo njiani kuonana na Mr. Linderman. Badala yake, wakatuna na mmoja kati ya washrika wake. Wakiwa na Micah kwenye chumba kingine, Niki anaambiwa amtishie kimapenzi mwanasiasa mmoja ambaye bwana Linderman anajishughulisha naye, ikiwa kama 'bima'.
Mwili wa Claire Bennet umelazwa juu ya meza huku afisa uchunguzi wa vifo akichungua ndani ya kifua cha Claire. Anachukua maelezo, afisa yule amegundua kwamba aliokotwa akiwa uchi na kuburuzwa hadi kwenye eneo la Red River Creek. Wakati afisa yule kaharibiwa mpango mzima na simu ya mkononi, Claire akajiponesha haraka-haraka na kuiba koti la maabara na kutoroka kimyakimya.
Viungo vya Nje
hariri- Watch "Collision" at NBC.com
- Collision at the Internet Movie Database
- Beaming Beeman: Episode 4: Come Together Director's blog on the filming of this episode.