Niki Sanders
Nicole "Niki" Sanders ni jina la kutaja uhusika uliochezwa na mwigizaji Ali Larter kwenye mfululizo wa televisheni wa Heroes. Niki ni mke wa D. L. Hawkins (Leonard Roberts) na ni mama wa Micah Sanders (Noah Gray-Cabey). Niki, anasumbuliwa na matatizo ya uwili-uwili, anaonekana kuwa na nguvu zaidi ya mwanadamu wa kawaida, kwa kuwa na uwezo wa kujigawa kuwa watu wawili. Awali, alikuwa na uwezo kutumia nguvu hizi wakati alter ego wake ("Jessica") akishika hatamu.
Niki Sanders | |
---|---|
muhusika wa Heroes | |
Mwonekano wa kwanza | "Genesis" |
Mwonekano wa mwisho | "Powerless" (yu-hai); "One of Us, One of Them" (-mekufa) |
Sababu | Ameuawa kwenye mlipuko wa jengo |
Imechezwa na | Ali Larter |
Maelezo | |
Majina mengine | Jessica Gina |
Ndoa | D. L. Hawkins (mume) |
Watoto | Micah Sanders |
Uwezo | Nguvu za ziada[1] |
Jina kamili | Nicole Sanders |
Tim Kring, mtunzi wa kipindi, alieleza ya kwamba awali alimuumba Niki akiwa na nguvu ya kuwa sehemu mbili kwa wakati mmoja, ambayo imetokana na maisha yake akiwa mama mlezi pekee.[2] Niki pia awali alitungwa awe kama msichana wa onyesho. Hata hivyo, Ali Larter hakuwa na umbo la kuweza kucheza uhusika wa msichana wa onyesho, hivyo basi uhusika ukabadilishwa na akawa kahaba wa mtandaoni.[3] Kwa mujibu wa watunzi Joe Pokaski na Aron Coleite, Niki alitolewa kwenye mfululizo na badala yake kawekwa Tracy Strauss hivyo Larter anaweza kucheza nyusika tofauti-tofauti, pindi walipogundua ya kwamba hawawezi kuendelea zaidi na uhusika wa Niki. Badiliko hilo lilipelekea kuweza kujua hadithi ya chimbuko lao, ambapo muhusika anagundua kwamba ana ngungu.[4]
Marejeo
hariri- ↑ Jensen, Jeff (2006-11-18). "Heroes: On the set of the hit that's saving the TV season". EW.com. uk. 6. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-07-24. Iliwekwa mnamo 2009-07-13.
- ↑ Standler (2007-02-07). "Heroes Execs discuss show's future, LOST, more". OgMog. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-02-27. Iliwekwa mnamo 2007-03-03.
- ↑ Caylo, Mel (2007-01-20). "TV Q&A: Heroes-Jeff Loeb". Wizard Universe. uk. 3. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-27. Iliwekwa mnamo 2007-01-26.
- ↑ Pokaski, Joe (6 Oktoba 2008). "Behind the Eclipse: Week 2". Comic Book Resources. Iliwekwa mnamo 2008-11-04.
{{cite web}}
: Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help)