Comair
Comair ni ndege iliyo na makao yake nchini Afrika Kusini. Makao ya ndege zake ni kwenye Uwanja wa ndege wa OR Tambo mjini Johannesburg pamoja na makao mengine kwenye nyanja za ndege za Cape Town na Durban.
Historia
haririNdege hii ilianza kufanya kazi mnamo 14 Julai 1946 kwa jina la Commercial Air Services. Ilianzishwa na AC Joubert, JMS Martin, L Zimmerman na JD Human. Safari za ndege kati ya Rand Airport, Johannesburg na Durban zilianza 1948, kwa kutumia ndege aina ya Cessna. Pamoja na safari hizi nchini Afrika Kusini, ilianzisha safari za nje ya nchi hadi miji kama Gaborone na Harare.[1] Kampuni hii iliwekwa kwenye soko la hisa la Johannesburg mnamo 1998. Ndege hii inamilikiwa na meneja (25%), makampuni na umma (52%), British Airways (18%) na wafanyikazi (5%). Hadi Machi 2007, ilikuwa na wafanyikazi 1,447.
Mnamo 2007, Comair ilianzisha kulula.com ambayo ni ndege inayosafirisha watu kwa bei rahisi.
Miji inayosafiria
hariri- Mauritius
- Sir Seewoosagur Ramgoolam International Airport
- Namibia
- Windhoek - Windhoek Hosea Kutako International Airport
- Afrika Kusini
- Cape Town - Cape Town International Airport
- Durban - Durban International Airport
- Johannesburg - OR Tambo International Airport
- Port Elizabeth - Port Elizabeth Airport
- Zambia
- Livingstone - Livingstone Airport
- Zimbabwe
- Harare - Harare International Airport
- Victoria Falls - Victoria Falls Airport
Ndege zake
haririHadi 25 Septemba 2009, Comair ilikuwa na ndege: [2]
Mdege | Juma | Oda |
---|---|---|
Boeing 737-200 | 3 | 0 |
Boeing 737-300 | 12 | 0 |
Boeing 737-400 | 7 | 0 |
Ndege | Jumla | Oda | Maelezo |
---|---|---|---|
Cessna 401 | 1 | 0 | |
Douglas DC-3 | 4 | 0 | |
Jumla | 5 | 0 |
Ajali
haririMnamo Nachi 1, 1998 ndege ya Comair Flight 206 ilipata ajali mjini Johannesburg na wasafiriwa wote 17 walikufa.