Safari (kutoka Kar. ‏سفر‎ safar) ni neno la kutaja mwendo au harakati ya watu kutoka mahali fulani kwenda mahali pa mbali angalau kiasi. Safari inaweza kufanywa ama kwa miguu au kwa chombo cha safari au usafiri fulani. Kama safari inazidi muda wa siku mmoja vituo vya safari yaani mahali ambapo msafiri anakaa au analala hadi kuendelea ni sehemu za safari yake. Kuna safari ndefu na safari fupi. Harakati inayotumia muda mfupi tu kama dakika chache au kwa umbali mdogo huitwi safari isipokuwa kwa lugha ya kutaania.

Matatu ni usafiri wa watu wengi nchini Kenya ndani ya miji lakini hutumiwa pia wa safari kati ya miji
Msafiri wa Unguja anakuta mabasi ya aina hii maarufu kama Chai Maharage

Kusudi la safari

hariri

Kuna kusudi mbalimbali la kufanyia safari kama vile kutembelea watu, biashara, kuhama kati ya mahali pa kazi na nyumbani, starehe na utalii. Kuna pia safari shauri ya uhamisho, kubadilisha mahali pa kuishi, ukimbizi, kuhiji, kutafuta tiba na kadhalika.

Vyombo vya safari

hariri

Tangu kale chombo cha kwanza cha safari kilikuwa miguu ya watu.

Baadaye watu walitumia wanyama kwa safari zao wakipanda punda, farasi au ngamia. Katika nchi pasipo na wanayama wa kufaa watu wenye mamlaka au wenye pesa walibebwa pia na watu wengine. Mifano ni sehemu za Afrika ya Kale ambako machifu na wafalme walibebwa au sehemu za Asia na Ulaya ambako wakubwa walibebwa kwa viti maalumu vilivyowekwa juu ya bao za kubebea na mara nyingi kufunikwa kama chumba kidogo.

Tangu kupatikana kwa barabara nyororo magari -ambayo yalijulikana tangu milenia ya 2 KK kama gari la vita au gari la kubeba mizigo- yalianza kutumika pia kwa safari zikivutwa na punda, maksai (pia ng'ombe), farasi an wanyama wengine. Safari kwa magari ya kuvutwa zilijulikana huko Roma ya Kale. Inajuwa na SUDANI, NIGERIAN na WAFRICA.

Katika nchi baridi sana penye theluji nyingi safari wa sleji zinazovutwa na farasi au pia mbwa ziko kawaida.

Tangu kupatikana kwa injini mbalimbali vyombo vya usafiri kama reli, motokaa, pikipiki au lori viliwazeshwa watu kusafiri haraka kushinda zamani. Ndege zimeongeza nafasi ya kusafiri kote duniani katika muda mfupi.

Safari kwa maji

hariri

Watu walioishi karibu na mito mikubwa, maziwa au kando la bahari walitembea kwenye maji kwa kutumia vyombo vya maji. Usafiri kwa maji hunawezesha kwenda mbali na kubeba mizigo kwa kutumia nishati kidogo. Vyombo vya usafiri tangu mwanzo vilikuwa maboti, mashua, mtumbwi, jahazi hadi meli.

Vituo vya safari

hariri

Wasafiri huhitaji mahali pa kukaa kwenye vituo vya safari zao. Hapa ni asili ya nyumba ya wageni na hoteli. Mtindo mwingine ni kusafiri na makazi ya kubebwa kama hema; mtindo huu ni wa kale sana ulitumiwa na wafuhaji wahamiaji tangu milenia nyingi lakini siku hizi imepatikana tena kwa njia ya camping ambayo ni aina ya safari za kitalii iliyoenea pande nyingi za dunia.

Neno "safari" katika matumizi ya kimataifa

hariri

Neno "safari" la Kiswahili limeingia katika lugha mbalimbali za Ulaya. Kwa kawaida hutumiwa kutaja safari ya kitalii katika Afrika kwa kusudi la kutazama wanyama pori. Mfano: "When we travel to Mombasa we will also have a three day safari to the Tsavo game park."

Tazama pia

hariri

Makala kuhusu neno "Safari" (si "Travel") katika wikipedia ya Kiingereza