Cyril Nyembezi
Mwandishi wa Afrika Kusini wa utaifa wa Kizulu
Cyril Lincoln Sibusiso Nyembezi (6 Desemba 1919 - 25 Juni 2000) alikuwa mwandishi, mwalimu na mhariri wa Afrika Kusini. Hasa aliandika kwa lugha yake ya Kizulu.
Nyembezi alizaliwa tarehe 6 Desemba 1919 eneo la Babanango nchini Afrika Kusini. Babake alikuwa mchungaji wa kanisa la Methodist. Alisomea Chuo Kikuu cha Witwatersrand mjini Johannesburg akapata shahada ya kwanza mwaka wa 1947 na ya pili mwaka wa 1954. Alimwoa Muriel mwaka wa 1950 wakawa na watoto wanne. Baada ya kufundisha lugha ya Kizulu katika vyuo vikuu vya Johannesburg na Fort Hare, akawa mhariri wa kampuni la Shuter na Shooter mjini Pietermaritzburg kuanzia mwaka wa 1959.
Maandishi yake
haririRiwaya
hariri- Mntanami! Mntanami! (1950; baadaye ikaitwa Ushicilelo lwesithathu tangu 1965)
- Ubudoda abukhulelwa (1953)
- Inkinsela yase Mgungundlovu (1961)
Mashairi
hariri- Imisebe yelanga (1963)
- Amahlunga aluhlaza (1963)
Mila za kijadi
hariri- Zulu Proverbs (1954)
- Izibongo zamakhosi (1958)
- Inqolobane yesizwe (1966; pamoja na Otty Ezrom Nxumalo)
Utafsiri
hariri- Cry, The Beloved Country, riwaya ya Alan Paton ikatafsiriwa kwa Kizulu kama Lafa elihle kakhulu (1958)
Uchunguzi wa kiisimu wa Kizulu
hariri- Uhlelo lwesiZulu (1956)
- Learn Zulu (1958)
- A Review of Zulu Literature (1961)
- Compact Zulu Dictionary (1964)
Angalia pia
haririMarejeo
hariri- Chapman, Michael. 2003. Southern African Literatures, University of Natal Press. ISBN: 1-86914-028-1
- ↑ "Nyembezi, C(yril) L(incoln) S(ibusiso) 1919-2000. Contemporary authors. 2004. Imeangaliwa tarehe 28 Desemba 2012 kupitia HighBeam Research Archived 21 Aprili 2016 at the Wayback Machine. (lazima kusajiliwa).
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Cyril Nyembezi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |