Daisy Bates

Mwanaharakati wa haki za kiraia wa Marekani

Daisy Bates (alizaliwa 11 Novemba 1914 - 4 Novemba 1999) alikuwa mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Marekani.

Faili:Daisy Gaston Bates.jpg
Daisy Bates

Maisha

hariri

Baba yake ni Hezakiah Gatson na mama yake ni Millie Riley. Alikulia kusini mwa Arkansas, katika mji mdogo wa Huttig, Arkansas. Hezakiah Gatson, alihudumia familia yake kwa kufanya kazi ya kukata mbao,katika kiwanda kidogo Cha kukatia mbao. Mama yake Millie Riley aliuawa wakati Daisy akiwa mdogo sana, na alilelewa na rafiki wa mama yake aliyejulikana kwa jina la Orlee Smith, aliyekuwa shujaa wa Vita ya kwanza ya dunia, na mke wake Susie Smith. Baba yake Hezakiah alimtelekeza, na Daisy hakuweza kumuona tena.[1] kwenye kifo cha mama yake. [2]Bates alikuja kutambua akiwa na miaka nane kuwa mama yake mzazi,alibakwa na kuuawa na wazungu watatu wa kiume, na mwili wake kutupwa kwenye dimbwi la maji, ambapo ilikuja kujulikana baadae.[3] Baada ya kujua kwamba hamna mtu aliyeshitakiwa kwa kifo Cha mama yake, ilimshtua na kumpa hasira baada ya kuona kuwa hamna haki iliyotendeka.[4] baba yake wa kumrithi ,Orlee Smith, alimwambia kuwa wauwaji, hawajawahi kupatikana na polisi hawakuonyesha jitihada ya kuwatafuta wauawaji. Nukuu "Maisha yangu sasa hivi ina lengo la siri ya kuwatafuta wanaume waliofanya hili tukio baya sana kwa mama yake". Alikuja kugundua mmoja wa wanaume aliyemuua mama yake. Alianza kuwachukia Wazungu. Bila kuwa na tumaini, baba yake wa kumrithi alimpa ushauri akiwa kwenye kitanda chake: Nukuu Alimwambia, umejawa na chuki. Chuki inaweza kukuharibu, Daisy. Usiwachukie watu weupe kwa sababu ni weupe. Kama unawachukia, hakikisha ina faida. Chukia unyanyasaji tunaofanyiwa hapa kusini. Chukia ubaguzi unaotunyima amani hapa kusini. Chukia ubaguzi unaotafuna nafsi ya kila mtu mweusi wanaume kwa wanawake.[5]< Bates alisema hajawahi kusahau hicho. Aliamini kuwa hiyo kumbukumbu inamsaidia kumpa nguvu katika uongozi wa haki za binadamu. Kabla ya kuambiwa ukweli kuhusu kifo cha mama yake, alikuwa akicheza na Beatrice, msichana wa kizungu aliyekuwa rika moja naye. Walishirikiana fedha kidogo walionayo na kuishi vizuri.[6] Daisy alikuwa na miaka 17 wakati alipoanza kuwa na uhusiano na Lucius Christopher Bates, aliyekuwa muuza bima, pia aliwahi kufanya kazi ya magazeti katika kusini na magharibi.[7] Lucius alitengana na mke wake wa Kwanza mnamo mwaka 1941 kabla ya kuhamia Little Rock na kuanza Arkansas State Press. Daisy na L.C. Bates walioana mnamo machi 4,1942[3] Mnamo mwaka 1952, Daisy Bates alichaguliwa kuwa rais wa Arkansas Conference ya NAACP branches.

Heshima na Tuzo

hariri

Alitajwa kuwa mwanamke wa mwaka mnamo mwaka 1957 na National Council of Negro Women. Arkansas General Assembly Commendatio ilimzawadia shahada ya Uzamivu ya Sheria katika chuo kikuu Cha Arkansas mnamo mwaka 1984. Shule ya Daisy Bates Elementary School katika Little Rock ilipewa jina hilo kwa heshima yake. Mnamo tarehe 11 April, 2019 serikali ya Asa Hutchinson walisaini katika Sheria mswada wa kumpitisha Daisy Bates na muimbaji Johnny Cash Kama wawakilishi wawili Wa mji wa Arkansas katika majimbo ya marekani National Statuary Hall Collection.[8]

Marejeo

hariri
  1. Martin, Douglas (4 Nov 1999). "Daisy Bates, Civil Rights Leader, Dies at 84". The New York Times.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Bates, Daisy. "The Death of My Mother". ChickenBones: A Journal. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-08. Iliwekwa mnamo 2011-04-02.
  3. 3.0 3.1 McCaskill, Barbara. "Bates, Daisy (1914–1999), civil rights activist, newspaper founder and publisher". American National Biography. Oxford University Press. Iliwekwa mnamo 27 Nov 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Bates, Daisy (Oktoba 11, 1976). "Interview with Daisy Bates". Southern Oral History Program Collection. Documenting the American South.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Calloway, Carolyn; Thomas and Thurmon Garner (Mei 1996). "Daisy Bates and the Little Rock School Crisis: Forging the Way". Journal of Black Studies. 5. 26: 616–628. doi:10.1177/002193479602600507. S2CID 145431981.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Stockley, Grif (2012). Daisy Bates: Civil Rights Crusader from Arkansas. University Press of Missi.
  7. Ethnicity, UALR Joel E. Anderson Institute on Race and; 2801 S. University Avenue Little Rock, AR 72204; race-ethnicity@ualr.edu, Phone:501 569 8932 Email; information, More contact (2018-04-30). "Meeting Ms. Daisy". Anderson Institute on Race and Ethnicity (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-05-25. Iliwekwa mnamo 2019-05-25.{{cite web}}: CS1 maint: numeric names: authors list (link)
  8. https://www.arkansasonline.com/news/2019/apr/11/daisy-bates-johnny-cash-statues-headed-us-capitol/
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Daisy Bates kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.