Danay García

(Elekezwa kutoka Danay Garcia)

Danay García (amezaliwa tar. 5 Julai 1984, mjini Havana, Kuba) ni mwigizaji filamu na tamthilia wa Kikuba. Kwa sasa anashiriki katika tamthilia ya Prison Break, na humu anacheza kama Sofia Lugo.

Danay García
Amezaliwa 5 Julai 1984 (1984-07-05) (umri 40)
Havana, Kuba

Wasifu

hariri

Maisha na sanaa (kwa ufupi

hariri

Danay Garcia alizaliwa na kukulia mjini Havana, Kuba.[1]. Aliazna kazi za unenguaji tangu yungali na miaka kumi.[2]. Danay anajua kucheza muziki wa Ballet, Salsa, Dansi ya Kiafrika, Merengue, Belly Dansi, na Flamenco. Baadaye akaja kuwa mwanamitindo. Kwa sasa, ni mmoja kati washriki wa mfululizo wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani cha Prison Break. Danay Garcia anaishi mjini Mexico City, na ana mume na watoto wawili.

Filamu alizocheza

hariri
Mwaka Jina la filamu Jina alilotumia Maelezo
2007 From Mexico with Love Maria
2007–2008 Prison Break Sofia Lugo Mfululizo wa TV
2007 CSI: Miami Camille Tavez Mfululizo wa TV
2006 Danika Myra

Marejeo

hariri
  1. "TV.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-08-25. Iliwekwa mnamo 2008-12-13.
  2. "Danay Garcia Bio - Danay Garcia Biography - Danay Garcia Stories". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-04. Iliwekwa mnamo 2008-12-13.

Viungo vya Nje

hariri