Dhamira
Dhamira (kutoka neno la Kiarabu) katika fasihi ni lengo, nia au kusudio alilolikusudia msanii wa kazi ya fasihi kufikisha kwa hadhira yake. Kwa mfano, msanii anaweza kutunga wimbo ambao ukawa unajadili madhara ya pombe. Hivyo, madhara ya pombe ni dhamira ya msanii huyo. Katika fasihi, dhamira zipo za aina mbili: kuna dhamira kuu na dhamira ndogondogo.
- Dhamira kuu ni lengo kuu lililomsukuma msanii wa kazi hiyo ya kifasihi kutunga kazi yake.
- Dhamira ndogondogo ni malengo madogomadogo yaliyochorwa na msanii wa fasihi ili kusaidia katika kufikisha lengo kuu.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dhamira kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |