Open main menu

Neno ni sehemu fupi ya lugha yenye maana. Ni sauti inayotamkwa au kuandikwa pamoja na kutaja jambo fulani.

Neno linaweza kuwa fupi lenye mofimu (yaani sauti inayowakilisha maana fulani) moja tu au kuwa ndefu lenye mofimu mbalimbali. Kwa kawaida ni mkusanyiko wa silabi kadhaa, zikiwemo konsonanti na vokali.

Wataalamu wanaona neno ni sehemu ya lugha yenye kituo kidogo mbele na nyuma yake, au kwa maandishi jumla ya herufi zenye maana zilizotengwa kwa nafasi nyuma na mbele.

Katika mazungumzo wakati mwingine si rahisi kutofautisha maneno kama ni maneno marefu au maneno mawili. Kwa mfano kuna maneno yaliyobuniwa juzi tu kwa kutaja mambo ya teknolojia na sayansi ambayo yanaunganisha maneno mawili kuwa moja:

  • garimoshi (gari + moshi) kama kifupi cha "gari la moshi" iliyokuwa kawaida zamani
  • mawasilianoanga (mawasiliano + anga - "telecommunication")

Si wazi mara moja kwa wakilizaji wanaosikia haya mara ya kwanza kama ni neno moja au maneno mawili.

Wataalamu wa lugha hutofautiana aina za maneno kama vile nomino, kitenzi, kivumvishi, kielezi, kiunganishi kiwakilishi na kihisishi

Maneno kwa pamoja yanaunda sentensi yakifuata masharti ya sarufi katika lugha.

Tazama piaEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Neno kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.